Mkoa wa Mwanza kupitia Kamati ya Mkoa ya Usimamizi wa Utekelezaji wa Mpango Kazi wa Taifa wa kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA) awamu ya pili (2024/25- 2028/29) umefanikisha kupunguza watoto waishio na kufanya kazi Mtaani katika kwa asilimia 50 hadi sasa.

Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Idara ya Mipango na Ufuatiliaji ya Mkoa huo Bw. Henry Mwaijega wakati akifungua kikao kazi cha kamati hiyo leo Januari 26, 2026 kwa niaba ya Katibu Tawala wa Mkoa huo chenye lengo la kupitia rasimu ya kitaifa na kutengeneza ya Mkoa.

Amesema tangu kamati hiyo izinduliwe mkoani humo imefanikisha Afua mbalimbali zikiwemo za watu wenye ulemavu na kufanikisha watu wenye ualbino 200 kupata vifaa saidizi na kujikinga na jua katika halmashauri za Misungwi na Kwimba vyenye thamani ya zaidi ya Milioni 200.

Aidha, amebainisha msaada mkubwa wa kamati hiyo katika kushughulikia Ukatili ambapo zaidi ya mashauri 250 yamefanyiwa kazi zitojanazo na Ukatili wa kijinsia, kutelekeza watoto na ukatili wa kingono katika kipindi cha julai -Desemba 2025.

Ameongeza kuwa wilayani Magu kamati hiyo kwa kushirikiana na viongozi wa halmashauri wamefanikisha kujenga kituo cha kushughulikia wahanga wa kijinsia (GBV One Stop Center) ambapo ni cha pili baada ya kile cha Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Sekou Toure.

Akihitimisha hotuba yake, Bwana Mwaijega ameendelea kuipongeza Kamati hiyo kwa kuwezesha mafunzo ya wataalam wakiwepo Jeshi la Polisi, Madaktari, Maafisa Ustawivwa jamii katika halmashauri ya Sengerema na kufanikisha usimamizi Shirikishi katika halmashauri za Kwimba na Buchosa.

Awali, akitoa utangulizi Afisa Ustawi wa Jamii Mkoa huo Baraka Makona ametumia wasaa huo ku kuwapongeza Mashirika ya SOS Children Village na KIVULINI kwa kuwezesha uzinduzi wa Mpango wa Kutokomeza Ukatili kwa Wanawake na Watoto (MTAKUWWA) mwezi Julai 2025.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.