Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe ametoa idadi ya watu waliopoteza maisha na miili iliyopatikana leo ni mwili wa mtoto mmoja Na kufanya idadi ya 228.
Bado Tupo kwenye eneo la ajali Ukara tukiendelea na uokoaji wa miili itakayopatikana ikiwa na chombo hiki kugeuza.
Japhet Masele Mtendaji Mkuu mpya wa TEMESA amewasili na Mpaka jana jioni tumeendelea kuangalia uwezekano wa kurejesha huduma katika eneo hili na tumepata injini inayoendelea kufungwa katika kivuko cha Mv. Ukara na saa 11 jioni itaanza mazoezi tayari kwa kuanza kutoa huduma wakati tunasubiri huduma ya kudumu na wananchi kuweza kuendelea katika shighuli zao za kiuchumi. Mv. Ukara inauwezo wa kubeba watu 70.
Wadau mbalimbali wanaoendelea kutoa rambi rambi leo hii waliotoa ubani ni pamoja na TPA wametoa Milioni 20, TPB Benki wametoa milioni 5.
Michango Kufikia saa 2 asubuhi Milioni 764,Fedha Iliyotumika 266 na Fedha iliyobaki benki 498.
Mkuu wa Jeshi la Wananchi Tanzania Jenerali Venance Mabeyo amesema jitihada za kukiinua kivuko zimefanikiwa mchana huu mnamo saa saba na nusu na sasa hivi kipo Wilma (Upright) kwani mwanzo kilikua kimelala kifudifudi,kisha jana kikalala ubavu na leo tumefanikiwa kukiinua na kuwa wima kazi iliyobaki ni kuondoa maji kwenye kivuko ili kiweze kuelea moja kwa moja ili kivutwe na kurudi nchi kavu. Anapongeza vyombo vya ulinzi na usalama katika ngazi zote, pia wenzetu waliotuunga mkono kampuni ya Mv Mkombozi kwa kuleta meli yao, GGM wameongeza nguvu ya vifaa, Songoro Marine na Orioni 2 Pamoja na wananchi.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.