Mkoa wa Mwanza unatarajia kunufaika na Tshs. Bilioni 7.8 za miradi ya kunusuru Kaya masikini kwenye Wilaya zake 7 inayotekelezwa na Mfuko wa hifadhi ya Jamii (TASAF).
Akizungumza leo na uongozi wa TASAF kutoka Makao Makuu, Viongozi waandamizi kutoka Wizara ya Fedha, Benki ya Dunia na Ubalozi wa Norway, Katibu Tawala wa Mkoa w Mwanza Ndg. Balandya Elikana amesema Serikali ya Mkoa itasimamia imara utekelezaji wa Miradi hiyo ili malengo yaliyokusudiwa yatimie.
"Serikali ya awamu ya Sita imejipambanua kwa vitendo kumletea maendeleo mwananchi, hivyo Miradi kama hii yenye tija kwa Wananchi hasa zile Kaya masikini tuna kila sababu ya kuona unakuja na majibu chanya". Amesisitiza Mtendaji huyo wa Mkoa.
Balandya amesema katika fedha hizo tayari Tshs Bilioni 3.3 tayari zimekuja na kuanza utekelezaji wake kwa kujengwa Miundombinu ya Madarasa, Ofisi, Vituo vya afya pamoja na Barabara.
Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii, Shadrack Mziray amesema tangu mfuko huo uanze kazi rasmi nchini mwaka 2001 zaidi ya Tshs Bilioni 400 zimetolewa zilenga kuinua kiuchumi kaya masikini na kumekuwa na matokeo mazuri kupitia mradi huo.
"Wilaya ya Misungwi ambayo tutakuwa na kazi ya siku mbili ya kupitia miradi mbalimbali tayari kuna wanufaika 600 ambao wametoka hatua ya umasikini hivyo kazi iliyo mbele yetu ni kuhakikisha kundi kubwa la Watanzania wanafikia malengo ya Serikali". Amesema Mziray.
Kwa upande wake mwakilishi kutoka Benki ya Dunia Wout Soveur amebainisha kuwa, licha ya kutolewa fedha hizo lakini itakuwa ni kazi bure kama wanufaika na Miradi hiyo hawapatiwi elimu ya kutosha kuanzia mpango wa Lishe bora na namna ya kujiongeza kipato cha familia.
Mpango wa kunusuru Kaya masikini ulizinduliwa Mkoani Mwanza Oktoba 2014 na kuanza kutekelezwa kwenye Wilaya zote Mkoani humo Julai 2015 ukiwa na jumla ya wanufaika 77,553.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.