MWANZA WAJIANDIKISHA KWA 63%, RC MTANDA ATOA WITO WANANCHI KUZITUMIA VIZURI SIKU 2 ZILIZOBAKI
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda amesema Mkoa wake umejipanga vizuri kuhakikisha zoezi la uandikishaji wananchi katika Orodha ya wapiga kura kwa ajili ya uchaguzi wa mamlaka wa Serikali za Mitaa linafikia malengo.
Amesema hayo leo tarehe 18 Oktoba, 2024 baada ya kujiandikisha katika daftari la orodha ya wapiga kura kwa ajili ya uchaguzi wa mamlaka wa Serikali za Mitaa 2024 katika Mtaa anaoishi wa Isamilo kaskazini B jijini Mwanza.
Aidha, amewataka Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri za Mkoa huo kuendelea kusimamia zoezi la uandikishaji wananchi kwa siku zilizobakia ili liweze kukamilika kwa amani na utulivu.
"Waheshimiwa Wakuu wa Wilaya wote na Wakurugenzi nawaagiza kuendelea kusimamia daftari hili kwa uhakikaka lakini pia kwa kufuata Sheria kanuni na taratibu zinazosimamia uchaguzi huu. Amesema Mhe. Mtanda
Sambamba na hayo amewataka wananchi kuendelea kujitokeza kwa wingi na kujiandikisha ili waweze kuchagua viongozi wazuri wa Serikali za mitaa watakaowaletea maendeleo katika mitaa yao.
Halikadhalika, Mtanda ametoa wito kwa vyama vya siasa kupeleka mawakala wa kusimamia zoezi la uandikishaji katika vituo na kushirikiana na serikali katika changamoto zinazojitikeza katika zoezi hilo.
Zoezi hilo la uandikishaji wananchi katika orodha ya wapiga kura kwa ajili ya uchaguzi wa mamlaka wa Serikali za Mitaa 2024 kwa Mkoa wa Mwanza mpaka sasa limefikia zaidi ya asilimia 63 kwa muda wa siku 7.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.