Mkoa wa Mwanza umeadhimisha kilele cha juma la elimu ya watu wazima lililofanyika Wilaya ya Ilamela katika viwanja vya shule ya Baptist.
Akiongea katika maadhimisho hayo Afisa Elimu Mkoa wa Mwanza Michael Ligola amesema Mkoa umeendelea kusimamia na kuratibu suala la Elimu ya Watu wazima na Elimu nje ya mfumo rasmi ambapo kwa upande wa MEMKWA Mkoa una jumla ya wanafunzi 3,402 kati yao wavulana ni 1,943 na wasichana ni 1,459.
"Mwaka wa kwanza jumla yao 2,244 wavulana 1271 na wasichana 973 na mwaka wa pili jumla yao ni 1,158 wakati jumla ya walimu ni 120 kati yao wanaume 57na wanawake ni 63 pia miongoni mwa walimu hao 118 ni walimu wa daraja A wakati 2 ni walimu wa kujitolea,"alisema Ligola.
Hata hivyo Ligola ameongeza kuwa Mkoa una vituo 26 vya ufundi stadi ambavyo vinatoa Elimu ya ufundi stadi kwa vijana 1375 waliomaliza elimu ya msingi na Sekondari kati yao wavulana ni 880 na wasichana ni 495 wakati fani zinazotolewa ni uselelmala,ufundi chuma,uashi,kompyuta,umeme, ushonaji na upishi.
Ikumbukwe kuwa kauli mbiu ya maadhimisho ya Juma la Elimu ya Watu wazima kwa mwaka huu ni "Kisomo kwa uendelezaji wa ujuzi".
Naye,Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza Bwana Christopher Kadio akimuwakilisha Mgeni rasmi ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongella amesema mtu yeyote mwenye dhamana ya kusimamia masuala ya elimu,na mdau yeyote wa elimu anapaswa kuhakikisha elimu katika ngazi zote inatolewa kwa ufanisi.
"Uzalishaji mali na utoaji huduma kwa sasa vinatawaliwa na matumizi makubwa ya maarifa,sayansi na tekinolojia ya kiwango cha juu katika mazngira haya suala la kujielimisha kwa kila mtu haliepukiki,alisema Kadio.
Aidha katika maadhimisho hayo Mgeni rasmi amekabidhi vyeti kwa wahitimu wa elimu ya watu wazima Mkoani hapa.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.