Usafirishaji wa mizigo kwenda ulaya wazinduliwa kwa tani 8 za minofu ya samaki kusafirishwa kwenda Brusels nchini Ubelgiji kwa kutumia ndege ya Rwada A330-300 yenye usajiri 9xR-WP.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa ndenge hiyo Waziri wa Ujenzi ,Uchukuzi na Mawasiliano ,Eng Isack Kamwelwe amesema kuna umuhimu wa kuwa na ndege ya ubebaji mzigo kutoka Mwanza kwenda Ulaya kwa kuwa Mwanza wanauwezo wa kuzalisha tani 200 za samaki kwa siku hivyo zoezi hilo limeanza rasmi leo na wiki ijayo ndege itarejea nchini.
" Miaka miwili iliyopita Rais wa Tanzania na Rwanda walikutana na kuzungumzia miradi mbalimbali na wakaona kuna umuhimu wa kuwa na ndege ya ubebaji mzigo kutoka uwanja huu kwenda Ulaya,juhudi za kutafuta ndege za mizigo ili kutimiza maagizo ya Rais wetu yametimia "anasema Kamwelwe
Ameongeza kuwa unapozalisha na kuuza nje, soko linapanuka na uchumi wa nchi kukuwa hivyo wameanza na vyakula baadaye matunda .
Naye Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega amesema kitendo cha kusafirisha minofu ya samaki na nyama kwenda masoko ya nje kupitia kiwanja cha Mwanza zitapunguza gharama za usafirishaji ,chakula kuwa fresh usafirishaji unapokuwa wa moja kwa moja ubora wa chakula unakuwa mkubwa tofauti na kusafirisha na kutatisha safari hadi siku nyingine kama ilivyokuwa awali hayo ni mambo muhimu ya kujivunia.
Aidha Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella amesema kiuchumi Mwanza ndio eneo la kati na kuwa chachu ya kukuza uchumi hivyo wananchi wawajibike na kufanya kazi na kuongeza nguvu katika uzalishaji, kuchangamkia fursa iliyojitokeza kwa kuwa mzunguko wa fedha utakuwa mkubwa sambamba na upatikanaji wa ajila utaongezeka.
"Mara ya mwisho ndege kubeba samaki ni 2008 leo tena tumeamka ni mapinduzi makubwa yameletwa na serikali ya awamu hii hivyo wawekezaji wachangamkie Mwanza ni mahali salama pakuwekeza biashara zao "anasema Mongella.
Kwa upande wake Meja Gen Charles Karamba Balozi wa Rwanda anasema leo ni siku muhimu baada ya kuyatekeleza maagizo ya Marais wawili hivyo wajibu wao ni kufanya kazi ili kuimarisha mawasiliano baina ya Tanzania na Rwanda .
"Ndio tumeanza kazi bado..lazima tufanye kazi kwa pamoja bidhaa iliyopo Tanzinia ni nyingi kutoka kwa wavuvi na wafugaji wajibu wetu ni kuifurahia hii kazi na kutaifanya ili kuleta tija na kukuza uchumi"anasema Karamba.
Katibu Mkuu Uchukuzi Dr.Leonard Chamuriho anasema wafanyabiashara watafute masoko ya nje kwa sababu vikwazo vyote vya kiufundi,mahitaji ya kukidhi viwango vya uhifadhi wa chakula na viwango vya usalama vyote vimekamilika hivyo wachangamkie fursa hiyo muhimu.
Aidha Meneja Rasilimali watu kutoka Tanzania Fish Processors Ltd Godfrey Samwel anasema mzigo pamoja na usafirishaji gharama zake ni USD 32000, mwanzo walikuwa wanasafirisha mzigo kupitia nchi jirani ya Kenya na walikuwa wakitumia gharama kubwa na muda mrefu hivyo kuwepo kwa usafiri huo kutawasaidia kwenda na wakati sambamba na kupunguza gharama.
"Tunaiomba serikali ijaribu kutafuta mashirika mengine ili tuweze kusafirisha nchi mbalimbali " anasema
Pascal Kalumbeta ni meneja wa uwanja wa ndege Mwanza anasema serikali imefanya uwekezaji mkubwa pamoja na kujenga jengo la mzigo la kisasa ambapo Mwanza kuna mazao ya samaki mengi hivyo ni wakati wa kuvutia wawekezaji na kutengeneza soko la kimataifa .
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.