Serikali imekuja na mpango mkakati wa kuzuaia na kupunguza ugonjwa wa malaria nchini,kwa kutoa elimu na hamasa ya kuzuia ugonjwa huo kupitia wataalamu wa afya.
Akizungumza katika semina ya kuzuia malaria nchini hapa kupitia serikali na wataalamu wa Wizara ya Afya hasa za mikoani,ambayo imehudhuriwa na wadau mbalimbali, Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza Ngusa Dismas Samike, alisema taratibu za kuzuia ugonjwa huu zianzie shule za msingi kupitia wataalamu wa afya .
Alisema vituo vya afya vyote nchini viwe na vifaa maalumu vya kutibia malaria hii itasaidia kupata na kukusanya takwimu sahihi ambazo zitasaidia nchi kuja na njia ambazo ni sahihi za kupambana na ugonjwa huu .
Aidha amesisitiza kuwa serikali itaendelea kufanya kampeni dhidi ya magonjwa nyemelezi kwajili ya afya za watanzania kwani maendeleo ya kupambana na kuzuia malaria yanachangiwa na serikali pamoja na shirika la afya duniani ( WHO) hivyo mpango mkakati huu lazima uwafikie watu wote nchini .
"Lengo hasa la mpango mkakati huu wa ni kufahamu wapi wamefanya vizuri na wapi wamefanya vibaya, namna ya kuzuia na kupambana nao kwa maeneo maambukizi yalipozidi ,mpango kazi huu utajikita katika maeneo mbalimbali ikiwemo Mara, Mwanza, Kagera, Kigoma, na Simiyu ili kuhakikisha ugonjwa huo unapungua kwa asilimia 1 sambamba na kuwafahamu wawekezaji wa mradi huu wa kuzuia malaria ambao ni pamoja na Global Fund." alieleza.
Aidha katika semina hiyo walieleza kuonesha asilimia 30.3 ya wagonjwa waliolazwa kutokana na ugonjwa wa malaria kwa mikoa yote hapa nchini huku viwango vya maambukizi kuwa asilimia 50 kutoka 14.8 asilimia kwa mwaka 2015. Vilevile viwango vya maabukizi kimikoa ni Kigoma 24 , Geita 17 , Mara 13, Kagera na Ruvuma 8 kwa mwaka 2021.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.