Maofisa Elimu,Wakurugenzi,Wakuu wa Shule ,Wakuu wa Vyuo na maofisa mbalimbali wa mkoa wa mwanza waanza maandalizi kwa ajili ya mapokezi ya wanafunzi wa kidato cha sita na ualimu .
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mapokezi hayo Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe.John Mongella amesema wakati huu ni wakuwa pamoja kuwasimamia watoto kwani Corona ipo lakini maisha lazima yaendelee .
Hivyo amewataka wakuu wa shule na vyuo kuhakikisha wanafunzi wanafanya mazoezi,maombi ili kuwajenga vijana kuwa imara na wanaojitambua ,kwani vita ya kukabiliana na ugonjwa huo ni kubwa ambapo Mhe. Rais alisimamia uzalendo na ukweli wenye dhamira ya dhati kwa uhai wa mtanzania na mstakabali wa maisha ya kila mmoja.
Mhe Mongella ameeongeza kuwa ofisi ya mkoa imeamua kukabidhi vifaa vya kujikinga na kudhibiti maambukizo ya ugonjwa huo ambavyo ni sanitizer,barakoa na seti za kunawia mikono ambayo ni matenki ya lita 200,mabeseni na ndoo kwa shule na vyuo vilivyopo mkoani humo.
Naye Afisa Elimu Mkoa wa Mwanza Martin Nkwabi anasema mkoa huo una jumla ya shule 37 za "Alevel" ambapo shule 18 ni serikali huku 19 ni za binafsi ambazo kwa ujumla zina wanafunzi 4,844 wa kidato cha sita,kwa upande wa wanafunzi wa ualimu kwenye vyuo vya Butimba na Murutunguru wana jumla ya wanafunzi 1,036.
Nicholaus Magige mkuu wa chuo cha ualimu butimba na Castory Mazula mkuu wa shule ya Sekondari Messa wanasema baada ya kupata maelekezo wamejipanga katika hatua za awali bila kuathiri matatizo ya kiafya ambapo wameondoa msongamano kwa kuwatawanya wanafunzi kukaa mbalimbali ata kwa wale wanaoishi bweni .
Pia upimwaji wa mara kwa mara utafanya kwa kila wanafunzi na watumishi hivyo jitihada za pamoja zinahitajika kutoka kwa walimu na wazazi ili kuweza kukabiliana na janga hilo.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.