Kamati ya maandalizi ya Lake Victoria Challenge imefanya kikao chake katika Ukumbi wa BOT Mwanza lengo ni kufanya maandalizi ya Shindano la Kimataifa la urushaji wa ndege ndogo isiyotumia Rubani (drone) Mkoa wa Mwanza.
Kikao hiki ni maandalizi ya mashindano hayo yatakayofanyika mwezi Novemba 2019.Benki ya dunia ikishirikiana na Mkoa wa Mwanza ndiyo waandaaji na kushirikisha Halmashauri za Mkoa,TCAA,TAA ,Shirika la Posta la Tanzania, kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa na wadau mbalimbali.
Lengo ni kuangalia ni kwa jinsi gani ndege hizi zisizo na rubani zaweza kutumika kutoa huduma za afya kuokoa maisha ya wananchi wa Mwanza, usambazaji wa vifurushi vidogo na barua sehemu zisizo kuwa na miundo mbinu rahisi pamoja na visiwani na milimani pamajo na kufahamu ni kwa jinsi gani ajira zinaweza tengenezwa pamoja na viwanda vidogo vidogo.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.