Mkurugenzi Mkuu wa kiwanda cha "MOTISAN Group" Bwana Shabani Petel ambaye ni mmiliki wa kampuni hiyo amewataka Wantania Kumuunga Mkono Mhe. Dkt.John Magufuli kwa jitihada zote anazozifanya ili kuhakikisha uchumi wa Mwananchi wa chini unaboreka.
Bwana Petel ameyasema hayo alipotembelewa na ugeni mkubwa wa Mhe. Rais Magufuli alipofika kufungua kiwanda cha Sayona kilichopo Nyakato Jijini Mwanza kilichojengwa kwa muda wa Mwaka mmoja na nusu kwa gharama za shilingi Bilioni 11 na milioni 800 tu.
Kiwanda hicho kinauwezo wa kuzalisha chupa 1200 kwa dakika moja katika mitambo yake minne na chupa 100 za maji na hii imepelekea kutoa ajira 200 kwa wazawa na kinaungana na kiwanda kingine cha Sayona kinachosindika matunda kilichopo mboga mkoani Pwani.
Bwana Petel amemuahidi Mhe,Rais Magufuli kuwa ifikapo Mwakani 2018 atakuwa ameanzisha viwanda vingine vitano ili kuunga Mkono juhudi kubwa zinazofanya na Mhe. Rais za kuifanya Nchi kuwa Tanzania ya Viwanda.
Aidha Mhe. Dkt. Magufuli amempongeza Bwana Petel kwa juhudi kubwa anazofanya kwa Kushirikiana na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongella.
Mhe. Dkt. Magufuli amempongeza Mhe. Mongella kwa juhudi kubwa anazofanya za usimamizi wa Sera ya Viwanda na kuhakikisha Viwanda vinaazishwa na vinaleta tija kwa Jiji la Mwanza na Watanzania kwa ujumla.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.