Mkoa wa Mwanza umezindua majaribio ya mashindano ya ndege zisizokuwa na rubani (drone) ikiwa ni sehemu ya kupunguza changamoto zilizopo kwenye maeneo yasiyofikika kirahisi.
Mhe.Nditiye amesisitiza kuwa ushindani utaangaliwa ubora,uimara, thamani,uwezo wa kubeba mzigo kwani itasaidia kwa kuwa kwa Afrika ni Tekinolojia mpya na kwa maeneo ya ukanda wa maziwa makuu imeanzia hapa Tanzania Mkoa wa mwanza,hivyo pongezi kubwa zimuendee Mhe.Mongella kwa ubunifu huu mkubwa alioufanya kwani yeye aliiahaanza kwa majaribio kupeleka dawa na vipimo kule Ukerewe na kuleta hapa Mwanza katika Hospitali mbalimbali ikiwepo Bugando.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga(TCAA) Mhe. Hamza Johari amesema kutakuwa na matumizi makubwa ya anga kwa shughuli za kuwaletea wananchi maendeleo kwani mwanzoni lilitumika anga moja tu,hivyo wamekaribisha tekinolojia hii kwa mikono miwili.
" Anga ni fedha, anga ni uchumi na anga inachagiza maendeleo, tumezoea kwa miaka mingi anga linalotumika ni lile la juu kwa maana ya ndege za abiria pamoja na mizigo ndizo huruka juu sasa tumepata tekinolojia nyingine ya ndege hizi zisizokuwa na rubani, hii imeleta wazo jipya la kutumia anga la chini," alisema Hamza.
Mhe.Hamza ameongeza kuwa hizi zitatumia mita 500 kutoka chini hadi mita 1000 ambapo lilikuwa halitumiki sasa tekinolojia hii imekuja ili na lenyewe litumike kwa shughuli za kiuchumi hasa zile sehemu zisizofikika kwa urahisi ili kuchagiza maendeleo kiuchumi.
Hata hivyo ameongeza kuwa ili kuto kuleta mkanganyiko wa anga lazima ndege zote(drone) zisajiriwe ili ajulikane aneyerusha ni nani na anuani zake ni zipi na ahughuli anazozifanya zina lengo gani,pia lazma apitishwe na mamlaka nyingine za nchi kama vyombo vya ulinzi na usalama, hapo ndipo taratibu ta TCAA zitaanza ikiwa ni pamoja na kutoruka juu zaidi ya futi 500 kwani kwa kwenda juu zaidi zitakutana na ndege nyingine na kwa kufanya hivyo inaweza kusababisha hatari kubwa zaidi,pia wasirushe sehemu zenye uwanja wa ndege hasa wa kimataifa wawe nje km5 na uwanja wa kawaida ni km 3 nje.
Aidha, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe.John Mongella ameishukuru Serikali ya awamu ya tano kwa kuruhusu tekinolojia hii mpya Tanzania na kidunia kwani mwanza imepata bahati ya kuwa kitovu cha mashindano hayo kwa Afrika Mashariki na kati kwani uzinduzi huu unafanyika Mwanza na haujafanyika Afrika.
"Kwa Mwaka kesho tukio lenyewe la mashindano litakuwa kubwa zaidi kwani litakuwa tukio la kidunia kwa mmeona mamlaka zote ziko hapa na wote hawa wanaona fursa hii kwani Mwanza tumeanza kupeleka dawa kwenye Visiwa vya Juma na Ukerewe ila si kwa ajili ya dawa tu, zinatumika kwenye sekta zote kama shirika la posta,"alisema Mongella.
Mhe.Mongella ameongeza kuwa atahakikisha kuwa kuna usalama wa kutosha na wenzetu wafanye kazi kwa amani na kuhakikisha kuwa tekinolojia hii haitishii usalama wa nchi na haina viatarishi kwenye jamii yetu na kuhakikisha inaongeza ubunifu na ushindani ili kuvutia wawekezaji mbalimbali katika nchi yetu na Afrika kwa ujumla.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.