Katika kufanikisha Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025 na Mpango wa Pili wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka Mitano (2016 – 2021) unaosisitiza ujenzi wa Tanzania ya Viwanda ili kuifikisha nchi katika uchumi wa kati ifikapo 2025.
Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF) ilipewa jukumu na Mkoa wa Mwanza kufanya utafiti na uchambuzi wa kina ili kubaini fursa za uwekezaji zilizopo katika Mkoa. Ili kukamilisha jukumu hilo, ESRF ilipata msaada wa kifedha kutoka Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) na kuanza kazi mara moja. Kazi ambayo ilifanyika kwa takribani muda wa miezi minne kuanzia mwezi Julai 2017 hadi Novemba 2017 kwa kushirikisha wadau kutoka Sekretarieti ya Mkoa na Halmashauri zote za Mkoa wa Mwanza.
ESRF ilifanikiwa kuandaa ripoti tatu ambazo ni Ripoti ya Fursafiche katika Viwanda (Industrialization Potentials Report), Ripoti ya Fursa za Uwekezaji (Investment Opportunities Report) pamoja na Mwongozo wa Uwekezaji ambao Mkoa umauzindua rasmi leo.
Dkt. Tausi Mbaga Kida, Mkurugenzi Mtendaji Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), katika Uzinduzi wa Mwongozo wa Uwekezaji Mkoani Mwanza amesissitiza kuwa ESRF ipo kwa ajili ya maendeleo ya nchi na wananchi wake na hivyo “msisite kututumia pale mnapohitaji msaada wa kitaalam. Uzinduzi wa Mwongozo huu ni mwanzo wa utekelezaji wake”.
Aidha ameongeza kuwa ESRF itafurahi kushirikiana na Mkoa katika kusaidia kufanya upembuzi yakinifu (Feasibilty Study) na kuandaa Business Plans kwa baadhi ya fursa ambazo Mkoa utapenda kuwekeza.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.