MWENGE WA UHURU KUKIMBIZWA UMBALI WA KILOMITA 68 SENGEREMA LEO
Halmashauri ya wilaya ya Sengerema, Mapema leo tarehe 17 Julai, 2023 imepokea Mwenge wa Uhuru ukitokea Buchosa tayari kwa kuukimbiza kwenye Miradi Saba yenye thamani ya zaidi ya Shilingi Bilioni 5.1
Akizungumza kwenye mapokezi yaliyofanyika kwenye Viwanja vya Bungonya, Mkuu wa Wilaya ya Sengerema Mhe. Senyi Ngaga amebainisha kuwa wamejiandaa vema kuukimbiza Mwenge wa Uhuru ambao unatarajiwa kufika kwenye miradi iliyoandaliwa kwa viwango bora.
Mhe. Mkuu wa Wilaya amefafanua kuwa Mwenge wa Uhuru uwapo wilayani humo utakimbizwa kwenye eneo la umbali wa KM 68 ardhini na kwamba wana ari na shauku kubwa ya kuukimbiza ili umulike na kuangaza miradi ya wananchi ya Maendeleo.
"Mwenge wa Uhuru utapokuwa kwenye Halmashauri yetu ya Sengerema utaweka Mawe ya Msingi kwenye Miradi Mitatu, utakagua Mradi mmoja pamoja na kufungua Miradi Mitatu yote ikiwa inang'ara na kupendeza." Amefafanua Shekideri.
Naye, Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru 2023 Ndugu Abdalla Shaib Kaim ameomba ushirikiano kwa Halmashauri ya Sengerema na akawataka kutokata miti, kutochoma misitu, kuacha uvuvi haramu, kuacha uchimbaji wa madini ambao unaharibu mazingira na kutofanya shughuli ndani ya Mita 60 kutoka kwenye vyanzo vya Maji ili kulinda kuhifadhi Mazingira.
Kaulimbiu ya Mbio za Mwenge wa Uhuru 2023 inasema "Tunza Mazingira, Okoa vyanzo vya Maji kwa Ustawi wa viumbe hai kwa Uchumi wa Taifa."
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.