MWENGE WA UHURU WAIPONGEZA BUCHOSA KWA UHIFADHI WA MAZINGIRA, WAPANDA MITI ZAIDI YA MILIONI MOJA KWA MWAKA
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru 2023 Ndugu Abdalla Shaibu Kaim ameipongeza Halmashauri ya wilaya ya Buchosa kwa juhudi kubwa wanazofanya katika kutunza na kuhifadhi mazingira.
Ndugu Kaimu ametoa pongezi hizo mapema leo katika shule ya Sekondari Bukokwa wakati akishiriki zoezi la upandaji miti 500 iliyotolewa na wakala wa huduma za misitu nchini (TFS) kati ya 1000 iliyopandwa kwenye shule hiyo katika kutekeleza ujumbe wa Mwenge wa mwaka huu.
Akizungumza baada ya kupokea taarifa amesema, viongozi na watendaji wameonesha kwa dhati nia ya kuhifadhi Mazingira kwani miti 1513700 imepandwa ndani ya kipindi cha mwaka mmoja wa 2022/23 katika maeneo mbalimbali kama kwenye miradi ya maji.
"Hongereni sana Buchosa, ninyi ni mabingwa wa uhifadhi wa mazingira." amesisitiza kiongozi huyo wa Mbio za wmenge wa uhuru zinazoenda sambamba na kaulimbiu isemayo
"Tunza Mazingira, Okoa vyanzo vya Maji kwa Ustawi wa viumbe hai kwa Uchumi wa Taifa."
Akitoa taarifa ya mradi huo, kaimu mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Walter Njau amesema Halmashauri hiyo imejikita katika kutunza vyanzo vya maji, kurejesha uoto wa asili na Ikolojia ya viumbe hai na utunzaji wa mazingira kwa kupanda miti ya aina mbalimbali ikiwemo ya matunda, miti ya mbao na miti ya asili.
Katika wakati mwingine, wakala wa maji na usafi wa mazingira Vijijini wilayani humo wameonesha nia ya kumtua mama ndoo kichwani wananchi zaidi ya 4118 kwa kuwaletea huduma ya maji safi kwa kuwajengea mradi wenye thamani ya zaidi ya milioni 190 ambao umewekewa jiwe la msingi (zaidi ya 85%) na Mwenge wa Uhuru ambao tayari umeshaanza kutoa maji.
Katika wakati mwingine, Halmashauri hiyo imedhihirisha shauku yao ya kutaka kuhifadhi vyanzo vya maji baada ya kuufikisha Mwenge kwenye mradi wa umwagiliaji unaolenga kuwanufaisha zaidi ya wakulima 700 kwa kupata chakula cha kutosha kabla ya kuzindua madarasa mawili Rwenchenga na kuweka mawe ya msingi kwenye bweni la wanafunzi Nyehunge.
Baada ya kushindwa kuzindua mradi wa jengo la huduma za dharula kwenye Hospitali ya wilaya kwa kukosa sifa za ubora na viwango stahiki kutokana na thamani ya fedha kiasi cha nilioni 300, Mwenge wa Uhuru umeiagiza Halmashauri ya Buchosa kujenga tabia ya kusimamia miradi vizuri ili iwe na tija kwa wananchi.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.