*MWENGE WA UHURU WAKABIDHIWA ILEMELA*
Mapema leo tarehe 14 Julai, 2023 Halmashauri ya wilaya ya Ilemela imeupokea Mwenge wa Uhuru ukitokea wilayani Ukerewe ambapo ukiwa wilayani humo utakimbizwa kwenye Miradi Sita yenye thamani ya zaidi ya Shilingi Bilioni 1.3
Akizungumza kwenye mapokezi yaliyofanyika kwenye Bandari ya Nyehunge, Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe. Hassan Masalla amesema wana ari nzuri na wamejiandaa vema kuukimbiza Mwenge wa Uhuru ambao unatarajiwa kufika kwenye miradi iliyotawanyika umbali wa Kilomita 57.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Ndugu Abdalla Shaib Kaim ameomba ushirikiano kwa Mkoa wa Mwanza hususani taarifa za miradi na nyaraka muhimu za miradi na uwepo wa Wakuu wa Idara ili kufanikisha vema mbio za Mwenge huo kwa mwaka 2023 wilayani humo.
Pamoja na kukimbizwa kwenye miradi, Mwenge wa Uhuru wilayani Ilemela unakagua shughuli mbalimbali za Upimaji Afya, Utoaji wa Elimu na Chanjo ya Uviko 19, Vipimo vya HIV pamoja na elimu ya upingaji rushwa na dawa za kulevya pamoja na elimu dhidi ya lishe bora.
Kaulimbiu ya Mbio za Mwenge wa Uhuru 2023 inasema "Tunza Mazingira, Okoa vyanzo vya Maji kwa Ustawi wa viumbe hai kwa Uchumi wa Taifa."
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.