Mwenge wa Uhuru umeingia Mkoani Mwanza ukitokea Mkoa wa Shinyanga na Kupokelewa na Katibu Tawala Mkoa Christopher Kadio kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe.John Mongella tayari kukimbizwa Halmashauri zote za Mkoa wa Mwanza.
Huku kukiwa na hamasa ya kutosha, wananchi wa Mkoa wa Mwanza wamepokea Ujumbe wa Mbio za Mwenge wa Uhuru wa 2019 kwa furaha kubwa uliotolewa na Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa usemao "Maji ni Haki ya Kila Mtu, Tutunze Vyanzo vyake na Tukumbuke Kushiriki katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa”.
Akitoa Taarifa ya Mkoa Kwa Niaba Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe John Mongella,Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza Christopher Kadio amesema, Katika kuhakikisha Maji ni Haki ya Kila Mtu, Mkoa wetu, hadi Februari, 2019 upatikanaji wa huduma ya maji safi umeongezeka toka asilimia 55 iliyokuwepo Machi, 2018 hadi kufikai asilimia 59 Februari 2019 kwa wakazi wote wa Mkoa wa Mwanza. Kati ya hao, wananchi wanaoishi vijijini huduma ya maji safi imeongezeka toka asilimia 48 hadi asilimia 49, na kwa wananchi wanaoishi mjini, huduma ya maji safi imeongezeka kutoka asilimia 80 hadi asilimia 81.
Aidha, ameongeza kuwa, Ili kutekeleza adhma hii katika Mkoa wa Mwanza, Serikali imetekeleza miradi ipatayo 91 ikiwa; mijini ni miradi 8 na vijijini ni miradi 83. Miradiya vijijini ina vituo vya maji vipatavyo 1,243 vyenye thamani ya Tsh. Bilioni 233.3 na uwezo wa kuhudumia watu wapatao 989,155 toka mwaka2015.
Aliongeza kuwa, mfano; Miradi 55 yenye thamani ya Tsh. 27.6 iliyo na vituo 875 yenye kuhudumia watu wapatao 437,500 imejengwa na kukamilika katika vijiji vya Halmashauri zote za Mkoa wa Mwanza.
Pamoja na miradi hiyo ya vijijini, ipo na miradi mikubwa ya maji na usafi wa mazingira mijini iliyojengwa na kukamilika katika miji ya Nansio na Sengerema yenye thamani ya Tsh. Bilioni 37.2 inayohudumia wananchi wapato 218,000.
Hata hivyo, pamoja na kukamilisha kujenga miradi tajwa hapo awali, Serikali bado inaendelea na kujenga miradi mipya mingine ya maji ya bomba vijijini ipatayo 28 yenye jumla ya vituo vya maji 366 vyenye thamani ya tsh. Bilioni 37.2 ambayo itahudumia watu wapatao 183,000 vijijini.
"Kwa upande wa mijini serikali inajenga miradi 4 yenye thamani ya Tsh. Bilioni 108.6 ikiwa ni ujenzi wa chanzo kipya cha maji Jijini Mwanza eneo la Butimba ambacho kitasambaza maji maeneo ya pembeni mwa Jiji yasiyokuwa na maji ya kutosha" alisema Kadio.
Aliendelea kuongeza kuwa, Uongozi wa Mkoa utaendelea kuhakikisha kwamba vyanzo vya maji vinatunzwa na kuhimiza wananchi wa Mkoa wa huo.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.