Mkuu wa Mkoa wa mwanza Mhe.John Mongella amepokea mwenge wa uhuru leo tarehe 26/08/2018 katika kijiji cha Izizimba " A " kilichopo Wilaya ya Kwimba ukitokea Mkoa wa Shinyanga baada ya kukabidhiwa na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe.Zainab R. Telack.
Akitoa salamu za Mwenge wa Uhuru katika kijiji cha Izizimba "A" Mhe. Mongella amesema Mkoa unaendelea kupambana na ugonjwa hatari wa Ukimwi chini ya kauli mbiu " Wananchi jitambue:pima afya yako sasa ," kwani maambukizi mapya yameongezeka kutoka asilimia 4.2 kwa mwaka 2014/2015 hadi kufikia asilimia 7.2 kwa mwaka 2017/2018.
"Juhudi zitafanyika kupunguza maambukizi mapya na kutoa tiba sahihi za magonjwa ya ngono na Tohara inayofanyika na wanaume ili kuwakinga wasiweze kupata maambukizi ya VVU kwa urahisi,"alisema Mongella.
Mwenge wa uhuru utakimbizwa jumla ya kilometa 831.3 na utafungua jumla ya miradi 56 katika halmashauri 8 ambayo imegharimu kiasi cha zaidi ya bilioni 13.7 katika miradi ya halmashauri yaKwimba,Magu,Misungwi,Sengerema,Ukerewe ,Buchosa,Halmashauri ya jiji,na manispaa ya Ilemela huku miradi hiyo ikiwa imechangiwa na serikali kuu, halmashauri,wananchi pamoja na wahisani mbalimbali.
Ikumbukwe kuwa uzinduzi wa mbio za mwenge wa uhuru ulifanyika Kitaifa Mkoani Geita tarehe 2 Aprili2018 na utahitimisha mbio zake tarehe 14.10.2018 Mkoani Tanga ambayo ni siku ya kumbukumbu ya baba wa taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Aidha kauli mbiu ya mwenge wa uhuru mwaka 2018 ni Elimu ni Ufunguo wa Maisha wekeza sasa kwa Maendeleo ya Taifa letu."
Hata hivyo Mwenge wa Uhuru 2018 umebeba ujumbe wa kudumu wa mapambano dhidi ya rushwa,mapambano dhidi ya madawa ya kulevya
na Ukimwi.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.