MWENGE WA UHURU WAZINDUA MADARASA 10 NG'HAYA SEKONDARI - MAGU
Leo alhamisi tarehe 20, 2023 Mwenge wa Uhuru umezindua vyumba kumi kumi (10) vya madarasa vilivyojengwa kwa shilingi milioni 200 kutoka Serikali kuu kwenye Shule ya Sekondari Ng'haya.
Akizungumza kwenye Uzinduzi huo, Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Ndugu Abdalla Shaibu Kaim ameipongeza Serikali kwa kuwajali wanafunzi na kuamua kuwajengea miundombinu hiyo ambayo itasaidia kupunguza msongamano darasani.
Ndugu Kaim amesema kutokana na miradi kadhaa iliyobainishwa shuleni hapo kama upandaji wa miti, utoaji wa elimu ya Lishe na mradi wa kuhifadhi mazingira kuhimili mabadiliko ya tabia nchi imeonesha dhamira ya dhati ya kuhakikisha wanafunzi wanajengwa kuwa wazalendo.
Akizungumza baada ya kuweka jiwe la msingi kwenye ujenzi wa wodi ya wazazi, wanaume, Stoo ya dawa na njia ya kutembea wagonjwa vilivyogharimu Shilingi milioni 750 Ndugu Kaim amewapongeza kwa usimamizi ambao utasaidia kupunguza msongamano wa wagonjwa hususani kwa wanaume kutoka 20 sasa hadi 100 pamoja na upandaji wa Miti ya matunda kuzunguka Hospitali hiyo.
"Mhe Rais ameonesha upendo mkubwa kwa makundi mbalimbali yakiwemo ya watu wenye ulemavu na anahakikisha wanapata mikopo kutoka fungu la 10% ya mapato ya ndani ili kuwawezesha kiuchumi, nawapongeza vijana kwa uzalendo kwani wamemaliza hadi marejesho" Ndugu Kaim wakati akizindua mradi wa vijana wafuga kondoo wenye thamani ya milioni 19 katika Kijiji cha Chandulu.
Katika wakati mwingine, Mwenge wa uhuru umeweka jiwe la msingi kwenye mradi wa ujenzi wa barabara ya RC Hostel yenye urefu wa KM 0.38 kwa thamani ya milioni 499 ambapo Ndugu Kaim ameagiza wakala wa barabara za mijini na vijijini (TARURA) kukamilisha kwa wakati mradi huo ili wananchi wapate huduma.
Kaulimbiu ya mbio za Mwenge wa Uhuru 2023 inasema "Tunza Mazingira, Okoa vyanzo vya Maji kwa Ustawi wa viumbe hai kwa Uchumi wa Taifa."
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.