N.C.U JENGENI NIDHAMU YA MATUMIZI YA FEDHA MLIZO REJESHEWA NA SERIKALI: RC MTANDA
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda leo Aprili 8, 2024 amewakabidhi rasmi uongozi wa chama cha Ushirika Nyanza akaunti yao Maalum maarufu kama ESCROW iliyo na zaidi ya shs bilioni 1 na kuwataka kufanya matumizi sahihi na yenye tija ya kuendeleza chama hicho.
Akizungumza katika hafla fupi iliyofanyika kwenye ukumbi wa Ofisi ya mkuu wa Mkoa, Mtanda amesema Serikali imekuwa na nia njema tangu ilipozuia matumizi ya fedha hizo mwaka 2018 na sasa baada ya kukamilika kwa mifumo ya usimamizi imezirejesha.
"Naomba niwe mkweli katika hili sitasita kuchukua hatua kali nitakapo baini kuna ubabaishaji wa matumizi ya fedha hizi,ni lazima kuwepo na mpango kazi wa matumizi yanayo lenga kukiinua chama hiki kikongwe",mkuu wa mkoa.
Amesema Serikali ya Rais Samia ina maono ya N.C.U inazidi kuwa chombo madhubuti cha kiuchumi hasa kutokana na wingi wa mali zake vikiwemo viwanda.
Naibu Mrajisi wa vyama vya Ushirika nchini Bw. Collins Nyakunga ameishukuru Serikali kwa kuitikia ombi la kurejeshewa akaunti hiyo na kuonesha imani kwa uongozi wa Nyanza kuja na mikakati madhubuti yenye kuleta mageuzi chanya ya kiuchumi.
"Mhe.mkuu wa mkoa Ofisi ya Mrajisi wa vyama vya Ushirika itaendelea kuwa karibu na N.C.U kuhakikisha kunakuwa na usahihi wa matumizi ya fedha hizi na tutasaidia kuwepo na ubunifu wa mipango ya kiuchumi,"Naibu Mrajisi
Mwenyekiti wa bodi ya chama cha Ushirika Nyanza,Benjamini Mikomangwa baada ya mali zote zilizouzwa kinyume na utaratibu kurejeshewa,ni wajibu wao sasa kuweka mipango yenye tija kwa chama hicho.
Tangu Serikali kuzuia matumizi ya akaunti ya chama hicho mwaka 2018 kwa muda wote huo ilikuwa chini ya usimamizi wa Ofisi ya mkuu wa mkoa wa Mwanza.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.