Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mhe.John Mongella ameongea na wanahabari kuutarifu umma wa wananchi wa Mkoa wa Mwanza kuhusu mapokezi ya Ndege Mpya na ya kisasa ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) aina ya “Boeing 787 – 800” Mkoani Mwanza Siku ya jumapili, saa 1:00 Asubuhi, tarehe 29 Julai, 2018.
Amefafanua kuhusu mambo yafuatayo kuhusiana na mapokezi ya ndege hiyo kubwa na ya kisasa:-
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Uongozi wa Mhe. Dkt John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika jitihada za kuboresha huduma za usafiri wa Anga na kuliimarisha Shirika la Ndege la Taifa (ATCL) ili kuinua uchumi wa Nchi yetu, Serikali imenunua Ndege mpya na ya kisasa aina ya “Boeing 787 – 800 Dreamliner”.
Ndege hiyo ikiwa kwenye safari yake ya kwanza Mkoani Mwanza aina ya “Boeing 787 – 800 Dreamliner” itapokelewa rasmi katika Uwanja wa Ndege wa Mwanza siku ya Jumapili tarehe 29 Julai, 2018 saa 1:00 Asubuhi.
Shirika la Ndege la Taifa (ATCL) kupitia ndege zake za “Boeing 787 – 800 Dreamliner” na “Bombadier Dash 8 – Q400” inafanya safari zake katika uwanja wa ndege wa Mwanza mara nne kwa siku kama ifuatavyo:-
Mwanza – Dar es salaam kupitia Kilimanjaro (Saa 3:20 Asubuhi – 5:40 Asubuhi – Dreamliner).
Mwanza – Bukoba (Saa 5:15 Asubuhi – 5:45 Asubuhi - Bombadier).
Mwanza – Dar es Salaam (Saa 7:15 Mchana – 9:00 Alasiri – Bombadier).
Mwanza – Dar es Salaam (Saa 2:20 Usiku – 3:40 Usiku – Dreamliner).
Amewajulisha wanahabari kuwa ndege hiyo “Boeing 787 – 800 Dreamliner” inayotegemewa kuwasili katika uwanja wa ndege wa Mwanza tarehe 29 Julai, 2018 ina uwezo wa kubeba abiria 262 (Daraja la kawaida “Economy” abiria 240 na Daraja la Biashara “Business” abiria 22).
Hadi sasa katika ndege hiyo itakayowasili siku Jumapili ya tarehe 29 Julai, 2018, tiketi 244 zimenunuliwa kwa safari ya ndege ya asubuhi na tiketi 158 zimenunuliwa kwa safari ya ndege ya usiku, hivyo natoa wito kwa wananchi wote kuchangamkia fursa kwa kuwahi kununua tiketi chache zilizobaki.
Mkuu wa Mkoa Amewaomba wananchi wote wa mkoa wa Mwanza na maeneo jirani tunawaomba wajitokeze kuja katika Uwanja wa Ndege wa Mwanza kushuhudia Mapokezi ya Ndege hiyo Mpya na ya kisasa aina ya “Boeing 787 – 800 Dreamliner”. Pia,amewaomba wananchi wote kuendelea kutumia usafiri wa ndege wa Shirika la Ndege la Taifa (ATCL) kwa ajili ya kuinua uchumi wetu na maendeleo ya Taifa letu.
Mwanza: Kazi na Maendeleo
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.