Uongozi wa Halmashauri ya Nyamagana Mkoani Mwanza umetakiwa kutoa elimu kwa wanufaika 2880 wa mpango wa kunusuru kaya masikini TASAF baada ya Serikali kutoa fedha Shs milioni 168.1 za kuinua uchumi kwa walengwa.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.Jenista Mhagama akizungumza na wananchi Wilayani humo mara baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa vyumba vya madarasa, Ofisi moja, Mabweni pamoja na bwalo la chakula kwenya shule ya Sekondari Nyamagana miradi inayofadhiliwa na TASAF amesema lengo la Serikali ni kuona uchumi wa mtu mmoja mmoja unapiga hatua ndiyo maana imekuwa ikitoa fedha nyingi kupitia miradi hiyo.
"Nataka kuona wanufaika wote 2880 wanaotarajiwa kupata fedha hizo wanaelimishwa vyema,h hizi fedha siyo za kunywea pombe bali zilete mageuzi ya kiuchumi kwa kufanya miradi itakayoongeza kipato ndani ya familia." Mhe. Mhagama.
Amebainisha kuwa mara baada ya kukagua Shule ya Sekondari ya Nyamagana ameziona kasoro ndogo ikiwemo udogo wa bwalo la kulia chakula na kuwataka walikamilishe na Serikali italeta fedha nyingine kati ya Juni au Julai mwaka huu ili lijengwe lingine kubwa zaidi.
"Mhe. Waziri sisi Nyamagana tunaishukuru Serikali ya awamu ya sita kwa namna inavyoonesha kutujali kwa vitendo,tupo mbioni kukamilisha ujenzi wa madarasa ya maghorofa kwa shule 13 na kila darasa litakuwa na wanafunzi 42 na tutakuwa wilaya yenye mfano hapa nchini kwa kuwa na shule bora".Amesema Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Mhe.Amina Makilagi.
TASAF imegharamia Shs Milioni 426,163,729.48 kujenga miundo mbinu shule ya Sekondari ya Nyamagana vikiwemo vyumba vya madarasa ya kidato cha tano na sita na hadi sasa zimetumika Shs milioni 258,904,204.29 na utekelezaji umefika asilimia 60.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.