Ofisi ya Mganga Mkuu Mkoa wa Mwanza yatoa Elimu ya Kipindupindu kwa Wanahabari
Ofisi ya Mganga Mkuu Mkoa wa Mwanza kwa kushirikiana na Wizara ya Afya zimeendelea na Mkakati wa kudhibiti Mlipuko wa ugongwa wa Kipindupindu ambapo leo wametoa elimu kwa vyombo vya habari.
Akizungumzia utoaji huo wa elimu uliofanyika kwenye ukumbi wa Ofisi ya mganga Mkuu wa Mkoa, mtaalamu wa elimu ya afya kwa umma kutoka Wizara ya afya Dkt. Emmanuel Mnkeni amesema jamii inahitaji kupata uelewa wa kutosha namna ya kuuepuka ugonjwa huo,dalili za mgonjwa na njia za kuudhibiti.
"Leo tupo hapa na vyombo vya habari kwa lengo la kuwajengea uwezo tukitambua umuhimu wa kalamu yao kwa jamii,kila mmoja akiwajibika kuweka mazingira katika hali ya usafi hasa vyoo mlipuko wa ugonjwa huu utatoweka," Dkt.Mnkeni
Amesema Kipindupindu kinatibika endapo mgonjwa atafikishwa mapema kwenye vituo vya afya mara baada ya dalili zote kubainika ambapo dalili kuu ni kuhara maji maji yanayofanana na yale ya kuoshea mchele.
"Ndugu zangu wana habari tujikite vyema katika kuelimisha jamii wakati mwingine wanaingiwa na taharuki bila sababu kama watakosa msingi mzuri wa elimu kuhusiana na ugonjwa huo," Leonard Charles,mratibu elimu kwa umma Ofisi ya RMO
"Tunashukuru kwa kupatiwa elimu hii,ushauri wetu kwa Serikali mamlaka zote husika ziwajibike ipasavyo kwani bado maeneo mengi miundombinu ya maji taka ni mibovu,"Wellington Masele,ITV
Grace Mbise kutoka Star Tv amebainisha bado baadhi ya makabila yanaendeleza mila zisizo na mashiko kwa kutochangia choo wenyewe kwa wenyewe kwa imani za kuepuka mikosi ndani ya familia na badala yake wanakwenda kujisaidia vichakani
"Tunapotumia maji ya visima tunatakiwa kuweka vidonge viwili vya Water Guard tofauti na maji ya bombani ambayo yanakuwa yamefanyiwa utaratibu wa kitaalamu kutoka kwenye vyanzo na unalazimika kuweka kidonge kimoja lakini tuzingatie kuchemsha maji hadi yatokote,"amefafanua Yusuph Seif Afisa afya kutoka Wizara ya afya.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.