OMBENI FEDHA SERIKALI KUU MMALIZIE UJENZI JENGO LA HALMASHAURI:RAS BALANDYA
Halmashauri ya wilaya ya Sengerema imetakiwa kuomba fedha iliyobaki Serikali kuu shs mil 369 ili kulikamilisha jengo la Halmashauri hiyo lililogharimu shs bilioni 3.5
Jengo hilo chini ya mkandarasi Suma JKT hadi sasa lipo nyuma ya muda kutokana na makabidhiano kutakiwa kufanyika Juni mwaka huu lakini imeshindikana kutokana na changamoto ya mifumo ya fedha.
Katibu Tawala wa mkoa wa Mwanza Ndugu Balandya Elikana akiwa katika ukaguzi wa miradi ya maendeleo wilayani humo amesema juhudi za haraka zifanyike ili fedha hizo zifike na kuanza kutoa huduma bora kwa wananchi.
"Mpango wa ujenzi wa jengo hili jipya ni baada ya kuonekana ufinyu wa jengo la zamani ambao unashindwa kutoa huduma sahihi kwa wananchi,hivyo mkurugenzi Bw.Binulu Shekidele hakikisha fedha hizo mnapata na huduma zote zitolewe humo",Katibu Tawala wa mkoa.
Mhandisi wa halmashauri hiyo Elias Mwita amebainisha ujenzi wa jengo hilo ulianza Machi mwaka 2023 na kutakiwa kukamilika mwaka huu lakini changamoto ya mifumo ya fedha na ubadilishaji wa mchoro wa ujenzi umechangia ucheleweshaji huo.
Hali kadhalika mtendaji huyo wa Mkoa ameagiza pia ujenzi wa nyumba ya Mkuu wa Wilaya inayojengwa na Ofisi yake kwa gharama ya zaidi ya shs milioni 400 ikamilike mwaka huu baada ya kuifanyia ukaguzi.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.