Kamati ya ufuatiliaji wa mradi wa ujenzi wa hospitali yenye hadhi ya mkoa wilayani Ukerewe imemtaka mkandarasi wa mradi huo kukamilisha ujenzi wa sakafu ya kwanza na kuanza sakafu ya pili mpaka ifikapo Februari 2, 2026 ili kupata nafasi ya kuendelea na hatua zingine za ujenzi.

Kamati imesema hayo leo Januari 17, 2026 katika kikao na mkandarasi mara baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa majengo ambapo ilieleza kutoridhishwa na kasi ya utekelezaji wa baadhi ya kazi.

Akimuwakilisha Mkuu wa Idara ya Miundombinu mkoa wa Mwanza, Mkadiriaji Ujenzi Godfrey Mwandoje amemtaka mkandarasi kuhakikisha anawasilisha vifaa mapema kwa mshauri wa wake ili vikaguliwe na kufanyiwa kazi za kukamilisha mradi ndani ya muda.

Sambamba na hayo Mkadiriaji Majengo Mwandoje amemsisitiza mkandarasi kufanyia kazi maelekezo yote anayopatiwa na kamati hiyo pamoja na yale yanayojadiliwa katika vikao mbalimbali wanavyokaa.

Mshauri wa Mkandarasi amemtaka mkandarasi kuhakikisha anaweka mazingira rafiki kwa wafanyakazi ikiwa ni sambamba na kuhakikisha majengo madogo madogo tanakamilika kwa haraka.

Halikadhalika Mkandarasi Msimamizi wa mradi huo wa Mhandisi Lucas Maganga amesema ndani ya wiki nne zijazo atakamilisha baadhi ya hatua ikiwa ni pamoja na jengo la mapokezi na kuweka umeme katika jengo la kuhifadhia maiti pamoja na kusakafia ukuta.

Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.