ONGEZENI BIDII KATIKA UTAFITI WAKULIMA WAPATE MBEGU BORA: RAS BALANDYA
*Awataka TARI kutoa mbegu kwa wingi na kwa wakati kwa wakulima*
*Apongeza kwa Utafiti utakaoongeza tija na mnyororo wa thamani kwa mazao ya Maharage,Mtama na Karanga*
Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza Balandya Elikana ameitaka Taasisi wa Utafiti wa Kilimo TARI kuongeza bidii katika jukumu lao ili kuwepo na tija kwa wakulima kupata mbegu bora wakati wote wa kilimo.
Akifungua leo mkutano wa Wadau wa mazao ya Maharage, Mtama na Karanga kwenye Hotel ya Gold Crest, Balandya amesema bado mkulima anakabiliwa na changamoto ya upatikanaji wa mbegu bora na kumrudisha nyuma katika malengo yake.
Amesema mikoa ya Kanda ya Ziwa ni maeneo mazuri katika uzalishaji na ufanyaji wa biashara hasa mazao ya Maharage, Karanga na Mtama hivyo mkulima anatakiwa kujengewa mazingira bora kuanzia Pembejeo na mbegu bora.
"Nawapongeza TARI na washirika wenu kwa kufanya utafiti na leo kuleta mrejesho, hii ni nafasi nzuri kuanzia kwa wafanyabiashara na wakulima kwani ni matokeo yatakayoongeza tija ya uzalishaji na mnyororo wa thamani," Balandya.
Meneja wa TARI Kanda ya Ziwa Mpoki Shimwela amebainisha Utafiti huo ulianza Juni mwaka 2023 kwa lengo la kuhakikisha wanapata mbegu bora itakayoweza kustahili ukame hasa kutokana na mabadiliko ya tabia nchi.
"Ndugu mgeni rasmi kwa kutambua umuhimu wa mazao haya wataalamu wetu wamefanya utafiti kwa kuwazungukia baadhi ya wafanyabiashara na tulichofanya ni kuboresha zaidi mbegu husika ili iwe na tija kwa mkulima",Mpoki.
Mkutano huo unawakutanisha Maafisa kilimo kutoka mikoa ya Kagera, Kigoma, Shinyanga, Tabora na Mwanza, Wafanyabiashara wa nataka na Taasisi za utafiti wa kilimo.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.