Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) imesema inataka zana ya Ugatuaji iwe na mamlaka ya kutekeleza shughuli zake kisera na kisheria.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa huduma za Sheria kutoka Tamisemi Edwin Mgendera kwenye mawasilisho ya wataalamu washauri katika kuboresha rasimu ya awali ya sera ya Taifa ya Ugatuaji wa madaraka kwa viongozi na wadau wa Mikoa mitano ya Kanda ya Ziwa (Simiyu, Mwanza, Kagera, Geita na Mara).
Mgendera alisema, ugatuaji sio jambo geni, awali ulikuwepo japo hapakuwa na sera wala sheria, hivyo walikuwa wanatekeleza shughuli hizo za ugatuaji wakitegemea andiko la ugatuaji wa madaraka la mwaka 1998.
“Tunataka kutengeneza sera ya ugatuaji wa madaraka kutoka serikali kuu kuja kwenye vyombo mbalimbali, inaweza kuwa wakala wa serikali, mamlaka ya serikali za Mitaa au watu Binafsi tofauti na pale awali unamuingizaje mtu binafsi kwenye suala la ugatuaji, tunataka sasa iwe kisera alafu sheria ifafanue,”alisema Mgendera.
Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Mhe. Dkt. Philis Nyimbi aliwataka viongozi ambao ni wawakilishi wa wananchi na wadau kutoka Asasi za Kiraia kutoa mapendekezo na maoni yatakayo boresha rasimu hiyo kwa maendeleo ya Taifa.
“Kila mmoja wetu anao mchango mkubwa wa kuleta wazo au kupendekeza ili mwisho wa siku Taifa letu lipate rasimu ambayo hata wananchi wakiisikia wataona vitu vimenyooka,ambavyo vimelenga asili yetu”alisema Dkt. Nyimbi.
Naye Juma Iddi kutoka idara ya Uratibu wa sekta Tamisemi alisema, ugatuaji madaraka umeleta mafanikio kidemokrasia na kwenye maeneo ya utoaji wa huduma ambayo Wizara za kisekta ziliwezesha mamlaka za msingi.
“Kwa sera ambayo tulikuwa nayo ilikuwa na mafanikio, wananchi wanashiriki vizuri katika shuguli za kidemokrasia za kuchagua na kuchaguliwa katika uongozi, wanajiongoza lakini pia katika utoaji wa huduma, Serikali inaweza kupeleka fedha moja kwa moja bila kupitia mahali pengine”alisema Iddi.
Aliongeza kuwz wanataka mafanikio waliyoyapata kwenye maeneo walioyagatua kama kwenye eneo la elimu wapate pia kwenye kilimo, mifugo na uvuvi na njia nzuri ni kuunganisha nguvu ya wadau wote kwakuwa na sera ya pamoja ili kila mmoja ajue wajibu wake.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.