Rais Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli awataka madereva na wananchi kulitunza liweze kudumu. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amezindua daraja la waenda kwa miguu la furahisha lilojengwa Jijini Mwanza kwa gharama ya shilingi za kitanzania 4.58.
Akihutubia wananchi wa Jiji la Mwanza waliofurika kushuhudia uzinduzi huo , Mhe. Rais Magufuli ameahidi kulitengeneza Jiji hilo kuwa kitovu cha utalii katika Nchi za maziwa makuu na Afrika nzima "nataka Mwanza iwe hurb ya afrika na kuendelea kupanua uwanja wa ndege wa Mwanza na utapanuka kwelikweli" ,Alisisitiza Rais Magufuli.
Amemuagiza Waziri wa Ujenzi, uchukuzi na Mawasiliana kufuatilia na kuhakikisha mkandarasi wa upanuzi wa uwanja wa ndege wa Mwanza analipwa fedha zote anazodai takribani shilingi za kitanzania Bilioni 9 ndani ya wiki hii ili aweze kuendelea na ujenzi na kukamilisha haraka ndani ya awamu ya tano.
Rais Magufuli amesema Mwanza imebadilika na itaendelea kubadilika na kuvutia wawekezaji na watalii wengi hususani uwanja wa ndege wa Mwanza utakapokuwa wa kitaifa na kuimarisha usafiri wa anga kwa kanda ya ziwa.
Rais Magufuli amewataka wananchi kulitunza daraja hilo la furahisha na kuwaonya madereva wasiozingatia sheria na kanuni na kuachana na tabia ya kuharibu miundombinu ya daraja na barabara.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.