RAIS SAMIA ANAWAPENDA WANANCHI WA KWIMBA AMEWALETEA MIRADI LUKUKI YA MAENDELEO : RC MAKALLA
*Ataja miradi wa ujenzi wa barabara kiwango cha lami Magu-Kwimba na Ngudu-Mabuki*
*Awataka watendaji Idara ya ardhi na wengine kuwasikiliza kwa staha na kutatua kero kwa wananchi*
*Asema Bilioni 1 imetolewa kujenga mradi wa maji Sumve*
*Awataka naafisa Ugani kutoa elimu ya kilimo bora kwa wananchi ili watumie mbegu na viuatilifu kwa wakati*
Leo tarehe 27 novemba 2023 Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. CPA Amos Makalla ameshinda na wananchi kwa zaidi ya saa 10 kwenye Viwanja vya Stendi ya zamani Ngudu kusikiliza na kutatua kero zao huku akisisitiza kuwa atawasikiliza wote wenye changamoto bila kumuacha hata mmoja.
Akifungua mkutano wake Mhe. Makalla amebainisha kuwa Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan inawajali sana wananchi wa Kwimba kwani imeleta miradi lukuki ya maendeleo ukiwemo ujenzi wa barabara ya lami ya Kwimba -Magu (Km 10).
Ameongeza kuwa pamoja na ujenzi wa barabara hiyo ambayo mkandarasi ameshapatikana, ameongeza kuwa Bilioni 1 imeletwa pia kujenga mradi wa maji kwenye jimbo la Sumve ambao umeshaanza kujengwa na umefikia asilimia 10 ya utekelezaji pamoja na miradi mingine mingi.
Hata hivyo, Mkuu wa Mkoa ameonesha kutokua na imani na Mkandarasi anayejenga jengo la kisasa la Makao Makuu ya Halmashauri kutokana na kusuasua katika ujenzi wake pamoja na uwepo wa fedha za ujenzi ambazo ameshapatiwa na kumtaka kujitafakari kabla hajachukua maamuzi mengine.
Aidha, amewataka watendaji wa idara ya ardhi na wengine halmashauri hadi kwenye ngazi za vijiji kuwa na ratiba yenye tija ya kusikiliza na kutatua kero za wananchi kwa wakati na kuhakikisha migogoro hususani ya ardhi inakomeshwa kwani kwa zaidi ya asilimia 80 ya kero zinazoibuliwa zimekua zikitoka kwenye sekta hiyo.
Halikadhalika, Mhe. Makalla awataka maafisa Ugani kutoa elimu ya kilimo bora kwa wananchi ili watumie mbegu na viuatilifu kwa wakati ili wapate tija na itaondoa tabia ya kulaumu serikali kuwa wanapewa mbegu, mbolea na viuatilifu feki wakati ni wao wanakosea wakati muafaka wa kutumia.
Awali Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe. Ng'wilabuzu Ludigija alifafanua kuwa amewasikiliza zaidi ya wananchi 400 na kwamba amebaini kuwa sekta ya ardhi imekua na migogoro zaidi hususani inayosababishwa na Mashamba ya urithi hivyo amewataka wananchi kufuata taratibu kwenye kuridhi mali ili kuepusha adha hizo na kwamba ofisi yake itaendelea na zoezi hilo.
Hata hivyo, Mhe. Ludugija ameahidi kuzifanyia kazi kero zote zilizoagizwa na Mkuu wa Mkoa ndani ya siku 14 na akawataka wananchi kutumia fursa zinazotolewa na serikali hususani wizara ya afya kupeleka watoto kwenye vituo cya kutolea huduma za afya kupata chanjo au dawa mbalimbali kwa ajili ya kuwakinga na kulinda afya za wananchi.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.