RAIS SAMIA MGENI RASMI TAMASHA LA BULABO, RC MAKALLA AWAALIKA WANANCHI KUMPOKEA
*Rais Samia kugagua Miradi ya kimkakati*
*Awataka viongozi kujiandaa na ugeni*
*Awakumbusha wakuu wa taasisi kutoa huduma bora*
Mkuu wa Mkoa wa Kwanza Mhe. CPA. Amos Makalla amewataka Wakuu wa taasisi na wananchi kujitokeza kwa wingi kumpokea Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye atawasili Juni 12, 2023 kwa ajili ya uzinduzi wa tamasha la Bulabo pamoja na kutembelea Miradi ya kimkakati iliyopo Mkoani Mwanza.
Mhe.CPA Makalla amesema hayo leo Juni 8, 2023 kwenye kikao kazi na Wakuu wa Taasisi zinazofanya kazi Mkoani Mwanza ambacho kimefanyika katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kikiwa na lengo la kupokea taarifa mbali mbali za miradi inayotekelezwa na taasisi hizo.
"Niwaombe Wakuu wa Taasisi pamoja wananchi wote wa mkoa wa mwanza kujitokeza kwa wingi katika kumpokea Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye tarehe 12, Juni 2023 atawasili Mkoani hapa na tarehe 13, Juni 2023 atakwenda kwenye uzinduzi wa tamasha la Bulabo na tarehe 14, Juni 2023 atatembelea miradi ya kimkakati," Amesema Mhe. Makalla
"Naomba kila Mkuu wa Taasisi auone ugeni huu kuwa ni ugeni wetu hivyo tunakila sababu ya kutoa ushirikiano kwa Mkuu wa Mkoa katika kutoa taarifa na ushirikiano wa hali na mali." Ameongeza Mhe. CPA Makalla.
Aidha, Mhe. Makalla ametoa rai kwa Wakuu hao wa Taasisi kuhakikisha wanatoa huduma bora kwa wananchi ili kusaidia mkoa kuwa katika hali ya usalama.
"Niwaombe muitumie ofisi yangu vizuri katika kuhakikisha tunatoa huduma bora kwa wananchi na hali ya ulinzi na usalama inakua shwari, wote tunategemeana katika kuhakikisha tunatoa huduma bora," Ameongeza CPA Makalla.
"Mimi Mkuu wa Mkoa ni kiongozi wa shughuli zote katika Mkoa huu nawaomba ushirikiano katika kutimiza majukumu tuliyopewa na Mhe. Rais,"Mhe. Mkuu wa Mkoa.
Pia, Mhe.Makalla ameitaka Bodi ya Pamba ikifikia msimu ujao wa maandalizi ya kulima na kuuza pamba changamoto zote zilizo ainishwa katika uwasilishaji zifanyiwe kazi ili msimu utakapoanza ziwe zimekwisha.
Naye, Mhandisi Paschal Ambros Meneja wa Tanroad Mkoani Mwanza amesema miradi wa kimkakati wa ujenzi wa daraja la JP Magufuli Lenye urefu wa kilomita 3 ukikamilika itainua maendeleo ya kijamii na kiuchumi katika Mkoa kwakuwa litaunganisha Wilaya za Misungwi na Sengerema, ambazo zimetenganishwa na ziwa.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.