RAS BALANDYA AHIMIZA KASI YA UKUSANYAJI MAPATO H/ZA BUCHOSA NA SENGEREMA
Halmashauri za Buchosa na Sengerema zimehimizwa kuwa na kasi ya ukusanyaji wa mapato ya ndani ili wazidi kuboresha huduma kwa wananchi na kupangilia mipango ya maendeleo kwa uhakika.
Rai hiyo imetolewa leo Juni 26,2024 kwa nyakati tofauti kwenye halmashauri hizo na Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza Bw Balandya Elikana wakati wa vikao vya Baraza la Madiwani kujadili hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali,CAG za mwaka wa Fedha 2022-23,amesema Halmashauri hizo zikiweka mkakati mzuri wa ukusanyaji mapato tija ya maendeleo kwa wananchi itazidi kuimarika.
"Nimesikia mlivyovuka malengo yenu ya ukusanyaji mapato hapa Buchosa kwa kuvuka zaidi ya asilimia 100,hongereni sana sasa ongezeni bidii kuanzia sasa ili muweze kuwa na miradi mingi ya kuwaletea maendeleo wananchi,"Balandya
Mtendaji huyo wa Mkoa amewataka pia Madiwani wa Halmashauri hiyo kusimamia vyema miradi ya maendeleo na kutoruhusi hoja za CAG kujirudia.
"Halmashauri ya Buchosa katika ukaguzi wa Hesabu za CAG mwaka 2022-23 walikuwa na hoja 6,tano za zamani na moja ya 2022-23 ambayo ipo katika utekelezaji,"Laban Kilulu,Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu Serikali
Akiwa kwenye halmashauri ya Sengerema iliyofikisha asilimia 86 ya mapato yake ya ndani Balandya ametoa maagizo ya kuhakikisha hoja zote zikamilishwe kwa wakati.
"Hesabu za CAG zinaonesha mmepata hati safi kwa miaka mitatu mfululizo na mlikuwa na hoja 17 na 16 mmezikamilisha na kubakiza 4 za nyuma ambazo nataka zikamilishwe,"Mtendaji wa Mkoa
Kuhusu madeni ya wazabuni ya zaidi ya milioni 400 amemtaka Mkurugenzi wa Halmashauri ya Sengerema kuongeza bajeti ya kuwalipa ili waweze kumudu shughuli zao
"Haiwezekani Mkurugenzi ukatenga milioni 50 ya kuwalipa wazabuni ni dhahiri utawapa umasikini kwa kushindwa kuwalipa kwa muda mrefu",amesisitiza Balandya
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Sengerema Mhe.Senyi Ngaga amebainisha maagizo yote yaliyotolewa watayafanyia kazi na hasa ukusanyaji mapato ya ndani.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.