RAS BALANDYA AHIMIZA MAONI BORA SERA YA UCHUKUZI KWA MAENDELEO YA TAIFA
Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza Ndugu Balandya Elikana leo Novemba 15, 2024 amefungua kikao cha kupokea maoni kuboresha sera ya uchukuzi na kuwahimiza washiriki kutoa maoni kwa uwazi yatakayoleta tija ya maendeleo nchini.
Akizungumza na washiriki hao kwenye ukumbi wa Rock City Mall Mtendaji huyo wa Mkoa amebainisha kuwa eneo la uchukuzi linalojumuisha usafiri na usafirishaji linagusa uchumi wa nchi hivyo mchango wa maoni yao utakwenda kuboresha sehemu zote zilizoonesha mapungufu.
"Nawashukuru Wizara ya Uchukuzi kwa kufanya zoezi hili, sisi hapa Mwanza yapo maeneo muhimu ya kiuchumi kama uwanja wa ndege, usafiri wa Meli na ule wa treni ya kisasa SGR yote hayo yanajitaji kupata muingiliano mzuri na Mataifa mengine ili kukuza uchumi wa nchi na maendeleo ya wananchi",Balandya.
Aidha amewataka washiriki hao kutoka makundi mbalimbali Serikalini na sekta binafsi kuona umuhimu wa sekta hii ambayo inachagiza ukuaji wa sekta nyingine ambapo mwaka 2022 ilikuwa kwa asilimia 3.80 na kuchangia pato la Taifa 6.70%.
"Sera ya mwaka 2003 baada ya kufanyika tathmini mwaka jana imegundulika na mapungufu kadhaa ambayo yanapaswa kufanyiwa kazi kwa lengo la kuboresha sekta ya uchukuzi,"Bi Devotha Gabriel, Mkurugenzi ufuatiliaji na tathmini, Wizara ya Uchukuzi.
Washiriki hao wanaotokea sekta ya usafiri na usafirishaji wanatoka mikoa ya kanda ya ziwa.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.