Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza Ndg.Elikana Balandya ameipongeza Wizara ya Fedha na Mipango kwa ubunifu wake wa kujenga Uchumi wa Nchi kwa kufanya majadiliano ya namna ya kutumia fursa zilizopo kwenye maeneo mbalimbali.
Akizungumza kwa niaba yake wakati wa kufunga mkutano wa kujadili mipango ya maendeleo mijini, Katibu Tawala Msaidizi Uchumi na Uzalishaji Emil Kasagara amesema Wizara ya Fedha na Mipango imekuja na mkakati huo wakati mwafaka kwani Mkoa wa Mwanza umejipanga kuhakikisha Uchumi wa bluu unachangamkiwa katika uzalizaji wa kisasa wa samaki.
"Serikali imeweka mazingira mazuri ya kuyawezesha makundi mbalimbali katika kujikwamua kiuchumi,hivyo ufugaji wa samaki kwa njia ya Vizimba wataendelea kuhimiza ili uwe na tija kwa Vijana kiuchumi."Amesisitiza Kasagara.
Amesema Mkutano huo wa siku mbili ambao umewahusisha wadau kutoka Mkoa wa Mwanza Wilaya ya Ilemela, Mkoa wa Tanga pamoja, Halmashauri zisizopungua 18 kutoka baadhi ya mikoa na Jumuiya ya Ulaya EU maazimio yote watakayokubaliana yatakuja na matokeo chanya katika maendeleo ya Taifa letu
.
"Huu ni mkakati wa Wizara ya Fedha na Mipango wa kuwakutanisha wadau kutoka Sekta mbalimbali zikiwemo Benki na kujadiliana kwa pamoja mipango ya maendeleo,changamoto zake na hatimaye kuyachukua maoni yao kwenda kuyafanyia kazi".Jonathan Mpuya mratibu wa miradi inayofadhiliwa kutoka nje , Wizara ya Fedha na Mipango.
Huu ni mpango wa miaka mitano unaofanywa na Wizara ya Fedha na Mipango lengo likiwa ni kumletea maendeleo mwananchi kupitia fursa mbalimbali zinazomzunguka.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.