Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza Ndugu Balandya Elikana amewataka maafisa usafirishaji (madereva na makondakta) kuboresha na kuimalisha huduma zao kwa wananchi kwakua sekta ya usafiri na usafirishaji ina mchango mkubwa katika kukuza uchumi wa mkoa.
Wito huo ameutoa leo Agosti 28, 2025 katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wakati akifungua Semina kwa maafisa usafirisha yenye lengo la kutoa elimu kuhusiana na maswala ya uwekezaji.
Aidha, amewasihi washiriki wa semina hiyo kutumia uwezo watakaojengewa waweze kuzitambua fursa za uwekezaji zilizopo katika sekta yao na kuweza kuendana na mabadiliko ya teknolojia.
“Niwaombe sana wadau katika sekta ya usafiri na usafirishaji kuendana na mabadiliko ya teknolojia ili kuwezesha na kuwa na manufaa makubwa katika sekta hii ya usafiri na usafirishaji”. Amesema Ndg. Balandya.
“Katika sekta hii kuna changamoto ya kukatisha ruti na kupeleka tunawasumbua abiria pamoja na bidhaa kwahiyo niwaombe tuachane na hii tabia ya kukatisha ruti”. Amesema Ndg. Balandya.
Naye, Meneja wa leseni kutoka LATRA Bw. Leo Ngowi amebainisha kuwa lengo kuu la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo wa kuendana na ukuaji wa Mji na ongezeko la watu katika Mkoa wa Mwanza.
“Kama tunavyofahamu Mkoa wa Mwanza unaongezeko la watu wengi kati ya miji inayoendeleakukua kwa kasi na serikali inaendelea kuwekeza katika sekta hii hivo ni lazima tuweze kujiandaa ili tuweze iuwahudumia watu ambao watakua wanaingia katika Mkoa wetu.
Semina hiyo kwa maafisa usafirishaji (Madereva na Makondakta) imeandaliwa na Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana Tanzania (CMSA).
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.