RAS BALANDYA AWATAKA WAZAZI/WALEZI KUONGEZA UMAKINI KATIKA MALEZI.
Walezi na Wadau wanaotekeleza afua za watoto wametakiwa kuzingatia malezi jumuishi ambayo ndiyo msingi wa asili wa malezi kwa watanzania.
Hayo yamesemwa na Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza Bw.Balandya Elikana mapema wiki hii wakati wa ufunguzi wa kikao cha kujadili utekelezaji wa afua za watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi kilichofanyika kwenye ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa mkoa Mwanza.
Balandya amesema malezi ya watoto zamani yalikuwa ya jamii nzima na ndio maana watoto walikuwa salama na wenye maadili.
"Niwaombe wale wote mnaowasaidia hawa watoto hakikisheni baada ya kuwatoa mtaani mnawaunganisha tena na wazazi wa kwa kuwa familia ndio mlezi wa kwanza kwa mtoto na baada ya hapo jamii inafuatia". Balandya.
Naye Irene Mwapembe kutoka Shirika la Railway Children amemuomba Mganga mkuu kuongea na wafanyakazi wake ili wapatiwe mafunzo kuhusu masuala ya ubakaji na utolewaji wa PF3 kwaajili ya manufaa ya watoto wanaofanyiwa vitendo hivyo.
"Katika eneo hili tumekuwa tukipata changamoto kutoka kwa wataalamu wa afya,wengine wanampima mtoto wanasema hakuna kitu na ukienda kwa mtaalamu mwingine anaona kuna kitu mtoto kafanyiwa"amesema Mwapembe
Kwa upande wake Afisa Maendeleo ya Jamii mkoa wa Mwanza Mwanza Janeth Shishila amewataka wadau wa watoto kuungana katika kutatua changamoto za watoto ili kuleta ustawi mzuri ndani ya jamii.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.