RAS BALANDYA AZITAKA HALMASHAURI KUZIMALIZA HOJA ZA CAG KWA WAKATI
Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza Balandya Elikana amezitaka Halmashauri za Wilaya ya Kwimba pamoja na Misungwi Mkoani humo kuhakikisha hoja za mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali CAG za mwaka wa fedha 2022 -2023 zinajibiwa na kufungwa ikiwa ni pamoja na utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika Wilaya hizo.
Ametoa kauli hiyo mapema leo Juni 25,2024 alipokua katika kikao cha ajenda za kikao maalumu cha baraza la madiwani cha kujadili hoja za mkaguzi na mdhibiti mkuu wa hesabu za serikali CAG kwa mwaka wa fedha 2023 /2024 huko Wilayani Kwimba na Misungwi.
"Niwaombe sana Menejimenti hizo hoja huwa zinajibiwa na kufungwa na haya mapendekezo ya CAG huwa hayajadiliwi huwa yatatekelezwa tu tuchukue kila hatua inayotatikana ili kutekeleza hayo mapendekezo ,Pia Waheshimiwa madiwani kuna hoja humu kama ya kutomakmilika kwa miradi mnawajibu wa kusimamia fedha zitengwe ili miradi ikamilike na kusaidia wananchi katika Wilaya zenu’’,amesema Balandya
Aidha Mtendaji huyo wa Mkoa amewataka watendaji kusimamia miradi ya maendeleo katika halmashauri zao ili iweze kukamilika na kuanza kutoa huduma kwa wananchi.
Awalia akiwasilisha taarifa za Ukaguzi wa hesabu za serikali kwa za Wilaya hizo mbili Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za Serikali Mkoa wa Mwanza Mustafa Shomvi amesema kwa muda wa miaka mitatu mfululizo Halmashauri hizo zimepata hati safi.
‘’Kwa mwaka 2022 -2023 Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba ilikuwa na hoja 19 kuhusiana na hoja za ukaguzi ambapo hoja zilizotekelezwa zilikua 12 ,hoja saba zipo katika hatua mbalimbali za utekelezaji, ’’amesema Shomvi
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Misungwi Johari Samizi ambae pia kwa sasa anakaimu Wilaya ya Kwimba amesema pamoja na Halmashauri hizo kupata hati safi kwa miaka mitatu akasisitiza watendaji kuendelea kufanya kazi kwa bidii.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.