Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza Bw. Balandya Elikana amewataka Maafisa elimu pamoja na wakuu wa shule kuhakikisha wanatenga na kuendeleza maeneo ya kilimo kwa ajili ya uzalishaji wa chakula cha wanafunzi ikiwa na lengo la kuimarisha upatikanaji wa chakula shuleni.

Amesema hayo leo Februari 10, 2026 katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza , wakati akizungumza katika kikao kazi cha kujadili na kutathmini afua za lishe ndani ya Mkoa huo, ambapo amesisitiza juu ya umuhimu wa mwanafunzi kupata chakula pale anapokua shuleni.

Bw. Balandya amesema shughuli za kilimo na ufugaji zitumike kama nyenzo za kujifunzia na chachu ya kuongeza uelewa wa lishe bora sambamba na kuongeza ushiriki wenye tija kwa kutoa motisha kwa wanafunzi wanaoonesha ubunifu na bidding katika maeneo hayo.

Aidha, amezitaka Halmashauri zote za Mkoa huo kusimamia utoaji wa fedha za lishe kwa wakati, ili kuimarisha utekelezaji wa mipango ya lishe mashuleni, huku akifafanua kuwa asilimia 50 ya fedha hizo zitumike katika ununuzi wa malighafi muhimu ikiwemo virutubisho kama matonel kwa lengo la kuboresha ubora wa chakula kinachotolewa kwa wanafunzi.

Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.