Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza Ngusa Samike ameahidi kuharakisha huduma za msingi kuwepo kwenye Kituo cha Hija Nyantakubwa kilichopo Wilayani Sengerema Mkoani Mwanza.
Katibu Tawala Ngusa amesema hayo mwishoni mwa wiki hii alipohudhuria Misa Takatifu ya Hija iliyofanyika eneo la Msalabani,amesema tayari eneo hilo limeshajengwa makazi ya Viongozi wa Dini kwa ajili ya kutoa huduma za kiroho hivyo atahakikisha mradi wa umeme unafikia eneo hilo.
"Nimesikia kuna changamoto ya upatikanaji wa mchanga mzuri wa ujenzi eneo hili, na eneo lenu mliopokuwa mnachimba kuna ujenzi wa Chuo cha Ardhi,naomba niseme tumelipokea na tutaenda kulifanyia kazi Mkoani." Katibu Tawala Mkoa.
Aidha katika salamu zake za Hija Katibu Tawala wa Mkoa Ngusa amewakumbusha Waumini kuyaishi vyema matendo ya kumpendeza Mungu hasa wakati wa mfungo wa Kwaresima kujinyima kwa dhati na kuwajali wanaotaabika na maisha.
Askofu wa Jimbo la Geita Mhashamu Flavian Kasala amesema Hija hiyo ya siku mbili ni nafasi muhimu kwa Waumini kumrudia Mungu na kuishi kwa amani na kusameheana.
Katika Misa hiyo Takatifu ilikwenda pamoja na zoezi la Harambee ya kuchangia ujenzi wa Kituo hicho cha Hija pamoja na nyumba ya Mapadre ,iliyoongozwa na Katibu Tawala wa Mkoa Ngusa huku Waumini wakihamasika na kutoa matoleo mbalimbali zikiwemo fedha taslimu na ahadi.
Kituo hicho cha Hija kipo eneo la Msalabani Parokia ya Nyantakubwa chini ya Jimbo la Geita kwa mujibu wa taratibu za Kanisa Katoliki.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.