RAS Mwanza ataka Elimu zaidi kwa wadau wa sekta ya uvuvi ili kulinda usalama wao majini
Leo Disemba 18,2023 Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza, Ndg. Balandya Elikana ameupokea Ofisini kwake ugeni kutoka Wizara ya Maji ukiongozwa na Katibu Mkuu wake Prof. Jamal Katundu ambapo katika mazungumzo mafupi Balandya ameshauri watumiaji wa Ziwa Victoria wazidi kuelimishwa hasa kutokana na kukabiliwa na majanga ya ajali za kuzama mara kwa mara.
"Mkoa wa Mwanza asilimia 53 ni Ziwa Victoria, hivyo idadi kubwa ya wananchi shughuli zao za kiuchumi wanategemea Ziwa hilo, hivyo watakapo elimishwa kuhusiana mazingira ya kiusalama nguvu kazi itazidi kuimarika," Balandya
Mtendaji huyo wa Mkoa ameupongeza mradi wa kituo cha usalama majini kinachojengwa Mkoani Mwanza na Jumuiya ya Afrika Mashariki na kusema kitaongeza tija kwenye sekta ya uvuvi na usalama wa majini kwa ujumla.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Prof. Jamal Katundu amebainisha lengo la ujio wake Mwanza ni kukagua na kutoa ushauri kwenye miradi mbalimbali iliyo chini ya bonde la Ziwa Victoria, Mwauwasa na kituo cha kimataifa cha usalama majini malengo yake yakiwa ni kuwanufaisha wananchi kama ilivyo kusudiwa.
"Ndugu Katibu Tawala wa Mkoa nikupongeze kwa kujaliwa miradi mingi hapa Mwanza,ni wajibu wetu sasa sisi viongozi tuhakikishe inakamilika kwa wakati,yenye ubora na kuwaletea maendeleo wananchi,"amefafanua Prof.Katundu wakati wa mazungumzo mafupi na mwenyeji wake.
.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.