Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza Ngusa Samike ameishauri Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba,TMDA kuongeza elimu zaidi kwa jamii kuhusiana na athari za matumizi ya bidhaa zitokanazo na Tumbaku.
Katibu Tawala wa Mkoa Ngusa akifungua kikao kazi cha kujadili utekelezaji wa shughuli za udhibiti wa bidhaa za Tumbaku Mkoani Mwanza, amesema bado Jamii inahitaji zaidi elimu hasa kutokana na vifo vinavyosababishwa na matumizi ya Tumbaku.
"Tunashuhudia madhara yatokanayo na uvutaji Sigara ni pamoja na Saratani ya Mapafu na afya ya kinywa pia inaathirika muweke utaratibu wa kuwafikia Jamii itasaidia kupunguza athari hizi"
Amesema kwa mujibu wa Takwimu watu Milioni 8 hufariki kila mwaka kutokana na matumizi ya bidhaa za Tumbaku,hii maana yake nguvu kazi ya Taifa inazidi kupungua ni wajibu tupambane kwa pamoja kuepukana na hali hii.
Meneja wa TMDA Kanda ya Ziwa Mashariki,Sophia Mziray amesema Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba inaendelea kuwakutanisha Wadau ili kukabiliana na madhara yatokanayo na matumizi ya Tumbaku.
Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Nelson Kamuhanda amebainisha bado kunahitajika elimu ya kutosha kutokana na athari za matumizi ya Tumbaku kumpata pia asiyetumia endapo atakutana na moshi wake.
Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba imekutana na Watendaji Kata pamoja na Wenyeviti wa Mitaa kutoka Wilaya za Nyamagana na Ilemela ikiwa leo ni Siku ya kutovuta Sigara Duniani ikitumia siku hii kuelimishana na kuona maeneo ya kuongeza juhudi ili Jamii iwe salama na athari ya matumizi ya Tumbaku.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.