RAS MWANZA ATOA RAI KWA WAFANYABIASHARA WADOGOWADOGO
*Awataka maafisa husika kushirikiana kikamilifu na kuwajibika katika kuwahudumia wafanyabiashara wadogo wadogo.
*awataka kufanya utambuzi na usajili na kutekeleza maagizo kwa kuzingatia mafunzo waliyopewa
Katibu Tawala wa mkoa wa Mwanza Ndg. Balandya Elikana leo Februari 16, 2024 amezindua mafunzo ya siku moja ya utambuzi, usajili na utoaji vitambulisho kwa wafanya biashara wadogowadogo mkoani Mwanza mfumo huo unaofahamika kama Wafanyabiashara wadogowadogo.
Akizungumza na maafisa Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wanawake na Makundi maalumu, maafisa biashara na maafisa Tehama pamoja na washiriki mbalimbali katika ukumbi mdogo wa Ofisi ya mkuu wa mkoa,Mtendaji huyo wa Mkoa amewataka Maafisa hao kuongeza juhudi ya uwajibikaji ili wafanyabiashara hao wapate fursa mbalimbali
Amebainisha hayo kutokana na kuwepo kwa idadi kubwa ya wafanya biashra wadogowadogo wambao hawatambuliki hivyo amewataka maafisa hao kuwasajili pamoja na kuwapa vitambulisho wafanya biashara hao.
“Tumekuwa na idadi kubwa ya wafanyabiashara wadogowadogo na Serikali imekuwa ikitoa maelekezo mbalimbali,agenda ya Serikali ni kuhakikisha wafanya biashara wanapatiwa fursa mbalimbali na mikopo pamoja na kuwatambua na kuwapanga ili wazidi kufanya biashara zao kwa urahisi” Amesema Balandya
Hata hivyo ameongeza kueleza umuhimu wa mafunzo hayo ambayo yamelenga kuleta mageuzi mbalimbali kwa wafanyabiashara huku akiwataka maafisa jamii hao kushirikiana pamoja ili kuweza kufanikisha zoezi hilo huku akiamini juhudi zao katika utendaji wao wa kazi
Nae Afisa maendeleo ya jamii,mkoa wa Mwanza Bi.Janeth Shishila ameeleza kuwa zoezi zima la mafunzo hayo ni kurahisisha utambuzi wa idadi ya wafanyabiashara, huku akiwahakikishia wafanyabiashara hao kuwa zoezi hilo halitakuwa na athari zozote katika jamii
“Zoezi hili linafaida kwa wamachinga wadogowadogo kwa kuanza kupata kanzi data na kufahamu walipo na shughuli wanazozifanya” Amesema bi. Janet
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.