RAS MWANZA AWAPONGEZA TAMSA KWA KUONA UMUHIMU WA MICHEZO
Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza Mhandisi Chagu Ng’homa amewapongeza Jumuiya ya Wanafunzi wanaosoma masomo ya Udaktari Chuo Kikuu cha Kikatoliki cha Afya na Sayansi shirikishi (CUHAS) Bugando kwa kuanzisha Bonanza la michezo (TAMSA CUP) ambalo linalenga kuimarisha afya.
Mhandisi Chagu amesema uwepo wa bonanza hilo utasaidia kuimarisha uwezo wa kujifunza na kuwakinga na magonjwa yasiyoambukizwa kwani muda mwingi wanautumia kwenye masomo hivyo bonanza hilo litawaondolea msongo wa mawazo.
“Ninajua muda mwingi mnakua busy na masomo na wakati mwingine mnakosa muda wa kushirikiana na wengine, hivyo kupitia bonanza hili litaimarisha pia mshikamano baina yenu”.
Aidha katika kuimarisha na kuendeleza Bonanza hilo Kaimu Katibu Tawala amewachangia kiasi cha shilingi laki tano ili kukuza na kuendeleza mfuko wa Bonanza hilo la TAMSA CUP.
Naye Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Dkt. Jesca Leba amesema michezo ni jambo muhimu kuzingatia licha ya Wanafunzi hao kuwa wanasoma masuala ya afya haimaainishi wao wako salama sana bali wanatakiwa pia kuhishughulisha na michezo kwani inawajengea uwezo na ufanisi darasani.
Ufunguzi wa michuano hiyo ya TAMSA CUP 2025 imefanyika katika Viwanja vya CCM Kirumba Wilayani Ilemela na imekua na kaulimbiu isemayo “Michezo kwa Afya Bora ya Akili”.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.