Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza Ngusa Samike amewataka wahusika wa Mikopo ya fedha asilimia 10 kutoka Halmashauri Mkoani humo kuyatumia vizuri mafunzo ya mfumo ili yawe na tija kwa walengwa na Taifa kwa ujumla.
Akifungua kikao kazi leo cha siku tatu kinachofanyika kwenye Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Samike amesema Serikali imechukua hatua mwafaka kuhakikisha kila mwenye sifa anafaidika na Mikopo hiyo hivyo wasimamizi wana wajibu wa kuhakikisha zoezi hilo linakuwa na majibu chanya.
"Mkasaidie Vikundi kuanzia namna ya kuandika andiko la Mradi, kubuni Miradi endelevu kama ufugaji wa Samaki wa kwenye Vizimba ambao una faida nzuri na tija" Samike.
Vilevile, amesema Serikali imenuia kuinua kipato kwa kila mwananchi yakiwemo Makundi ya Vijana, Wanawake na Watu wenye Ulemavu na wajibu wa Serikali ni kutekeleza Sera ili kuleta Maendeleo kwa ujumla.
Mratibu wa Mafunzo hayo kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Idara ya Maendeleo ya Jamii, Bi. Janeth Sishilla amesema utaratibu huo wa mfumo wa usimamizi wa Mikopo ya asilimia kumi utaanza Julai Mosi wakiwa na matarajio chanya kutokana na mfumo huo kudhibiti wale watakaojaribu kwenda kinyume na utaratibu huo mpya.
Wahusika na Mafunzo hayo ni Wakurugenzi wa Halmashauri, Waweka hazina, Maafisa Mipango, Maafisa Maendeleo ya Jamii wa Halmashauri, Maafisa Tehema wa Halmashauri na Waratibu wa Mikopo ya asilimia 10 wa Halmashauri.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.