RAS MWANZA AWATAKA WALIMU KUSIMAMIA MIONGOZO YA USIMAMIZI WA ELIMU ILI KUINUA UFAULU
Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza Ndugu Kusirie Swai ambaye ni Mkuu wa Seksheni ya Usimamizi, Ufuatiliaji na ukaguzi amewataka Maafisa Elimu na Walimu Mkoani humo kusimamia miongozo ya sekta hiyo ili kuinua ufaulu Mkoani humo.
Ndugu Swai ametoa wito huo kwa niaba ya Katibu Tawala Mkoa leo Januari 23, 2024 kwenye kikao cha tathmini ya utekelezaji wa shughuli za Elimu kwa 2023 na kuwekeana mikakati ya ufanikishaji kwa 2024.
Swai amesema katika kuhakikisha Sekta ya Elimu inaimarika ni lazima kutekeleza vyema mtaala mpya wa elimu ambao umeanza kutumika mwaka huu na kwamba katika kufanikisha hilo walimu wanapaswa kupewa mafunzo angalau kila robo mwaka.
"Ufaulu wa mkoa wa Mwanza umepanda kwenye kila mitihani katika matokeo ya kidato cha nne na kidato cha pili, lakini bado lugha ya kiingereza bado haijapewa kipaumbelee sana katika shule za Msingi na Sekondari ", Ndugu Swai.
Suala la chakula shuleni ndugu Swai amelitaja kuwa linasaidia sana kuthibiti utoro wa wanafunzi hivyo akatoa wito kwa walimu kushirikiana na wazazi katika kufanikisha suala hilo muhimu kwa maendeleo ya Taifa.
"Wazazi waendeelee kuelimishwa kuchangia xhakula shuleni, Maafisa Elimu halikisheni mnaimarisha menejimenti za shule za Msingi, Secondari na katika ngazi zote kila wakati na kuimarisha ufatiliaji wa jambo hilo." Amesema Kaimu Katibu Tawala huyo.
Aidha, Swai ametoa wito kwa Wakurugenzi wa Halmashauri kuhakikisha wanasimamia ujenzi wa miundombinu ili iwe bora na kuondosha kabisa tatizo la uhaba wa madarasa, matundu ya vyoo, maabara, mabweni pamoja na samani.
Naye, Mthibiti Mkuu wa ubora wa elimu kanda ya ziwa Mwalimu Lucy Nyanda amewataka wadau wa kikao hicho kuhakikisha wanazingatia maagizo yatolewayo ili kwenda kuboresha utendaji wa kazi kwenye maeneo yao.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.