RAS MWANZA AWATAKA WATENDAJI SEKTA YA AFYA KUTEKELEZA VEMA PROGRAMU YA DREAMS KUSAIDIA VIJANA KUTIMIZA NDOTO ZAO
Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza Emil Kasagara ametoa rai kwa watendaji wa Halmashauri za Mwanza kutekeleza Ipasavyo Programu ya DREAMS ili kusaidia kutimiza ndoto za watoto na vijana walio katika rika balehe ili kuokoa kizazi cha sasa na baadae dhidi ya maambukizi ya ukimwi
Ndugu Kasagara amesema hayo leo Machi 14, 2024 wakati akizindua rasmi kwa niaba ya Katibu Tawala Mkoa Programu ya DREAMS inayoratibiwa na KKKT Makao Makuu kwa ufadhili wa Shirika la msaada la Marekani USAID. Programu itakayotekelezwa katika Halmashauri 7 za Mkoa wa Mwanza.
Ndugu Kasagara amesema Mkoa huo unapongeza juhudi hizo na kuupokea kwa dhati programu hiyo na kwamba Ofisi hiyo itatoa ushirikiano wa dhati kuhakikisha unafanikiwa ili kuwa na jamii yenye afya njema yenye kujihusisha na uzalishaji mali na kujenga uchumi.
Bwana Issa Murshid Mkurugenzi mshiriki wa Kanda wa mradi wa USAID Kizazi Hodari (Brave Generation) amebainisha kuwa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) linatekeleza Programu hiyo chini ya ufadhili wa USAID ili kuhakikisha vijana wanalindwa na kuwa na Taifa lenye nguvu kwa maendeleo ya Taifa.
Awali, mratibu wa programu ya DREAMS kutoka TACAIDS Ndugu Kelvin Kisoma amefafanua kuwa mradi huo umelenga kusaidia vijana wa rika la miaka 10- 24 ili kuwalinda kwenye hatari ya kupata maambukizi ya ukimwi hivyo wanapata afua zitakazowasaidia kujilinda kwani ni kundi lililo kwenye hatari ya kuambukizwa.
Vilevile, amebainisha pia kwamba tafiti zilizofanywa mwaka 2016/17 zilionesha kuwa kundi la vijana lilipata na maambukizi mapya kwa 40% na kufanya kuwa sawa na kila kwenye kundi la watu kumi wanne wanaweza kuwa na maaambukizi. Pia alieleza kuwa watoto na vijana wakiwa katika hatari zaidi ya kupata maambukizi mapya.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.