Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mhe. Mhandisi Robert Gabriel amewakaribisha wawekezaji wakubwa kukamata fursa za uwekezaji zinazopatikana Mkoani humo ikiwemo ujenzi wa Hoteli za Kitalii fukwe za Ziwa Victoria na ufugaji wa samaki wa Vizimba.
Ametoa wito huo mwishoni mwa wiki hii kwenye mkutano wa mtandao thabiti kwa ukuaji endelevu wa biashara, ulioandaliwa na Benki ya NMB Mkoani Mwanza na kuwakutanisha wafanyabiashara wakubwa ambapo amesema Jiji hilo lipo sehemu ya Kimkakati kutokana na kupakana na Mataifa ya jirani na kuwa kitovu cha Biashara.
"Tuna kila sababu ya kujikita katika uchumi wa buluu, Samaki wetu wana soko zuri huko barani Ulaya hivyo tuchangamkie fursa ya Ufugaji" Mhe Gabriel
Vilevile, amesema Jiji la Mwanza bado lina nafasi kubwa ya Uwekezaji wa Hoteli za hadhi ya Kimataifa ufukweni mwa Ziwa Victoria na kusisitiza milango ipo wazi ya ushirikiano kati ya Ofisi yake na wale watakaokuwa tayari kwa Uwekezaji huo.
Mkuu wa Idara ya Biashara kutoka Benki ya NMB Alex Mgeni amesema Taasisi hiyo imezidi kupiga hatua kutokana na kuweza kumkopesha mteja zaidi ya Shilingi Bilioni 200.
Katika mkutano huo na wadau, Benki hiyo imetoa mada mbambali kutoka kwa Wataalam wake kuhusu kazi za kibiashara na wateja wake na jinsi wanavyokabiliana na kuzifanyia kazi changamoto zinazojitojeza.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.