RC MAKALLA:TAMASHA LA BULABO MWANZA KUFANYIKA Juni 13,2023
*Chifu Hangaya kuwa mgeni rasmi.
*Ataka hamasa kubwa kufanikisha Tamasha*
*Ahimiza Utamaduni wa Wasukuma kuenziwa
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. CPA. Amos Makalla na Katibu Tawala wa Mkoa huo Ndg. Balandya Elikana leo Juni 7, 2023 wameshiriki kikao cha maandalizi ya Tamasha la Utamaduni la wasukuma (BULABO) ambalo limeandaliwa na kituo cha utamaduni cha Bujora pamoja na Watemi.
Akizungumza na kamati ya maandalizi ya Bulabo kwenye ukumbi mdogo wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa,Mhe.Makalla amewakikishia kushirikiana nao bega kwa bega ikiwemo upatikanaji haraka wa fedha za kufanikisha tamasha hilo ili kufana zaidi.
"Nawaomba sana tushirikiane vyema kwa kulitangaza ili watu wapate hamasa na kujaa kwa wingi",amesisitiza CPA Makalla
Tamasha hili linalenga kuenzi na kudumisha urithi na utamaduni wa Mtanzania hususani wa kabila la Wasukuma na kusheherekea mavuno.
Tamasha hilo anatarajiwa kulifungua Chifu Hangaya ambaye ni Rais Mhe. Dkt.Samia Suluhu Hassan
Tamasha hilo linalofanyika kila mwaka lilianza rasmi mwaka 1955.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.