RC MAKALLA AMALIZA MGOGORO WA PAROKIA YA KAGEYE
*Aruhusu waumini kusali kama zamani*
*Asema kwa nyaraka kageye ni makumbusho ya Taifa*
*Aomba viongozi wa serikali kushirikiana na kanisa*
Mkuu wa Mkos wa Mwanza Mhe.CPA.Amos Makalla ameumaliza mgogoro baina ya Kanisa Katoliki na Halmashauri ya Magu kwa kuwaruhusu Waumini kuendelea kusali eneo la kihistoria la Kageye.
Akizungumza leo na uongozi wa Halmashauri na kanisa Katoliki, baadhi ya wananchi mara baada ya kutembezwa na kufahamishwa taarifa za kihistoria kwenye eneo hilo, Mkuu huyo wa Mkoa amebainisha amefanya mawasiliano na mawazili wa Maliasili na Utalii na Wizara ya Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi,hivyo kwa hatua ya kwanza ameruhusu Waumini kuja kusali hapo.
"Hili eneo ni la Mali Kale chini ya Makumbusho ya Taifa, baada ya mwaka 2019 kufanyika mabadiliko,hivyo nawaomba waumini endeleeni kuonesha ushirikiano na Serikali wakati mchakato wa namna ya kulitumia eneo hili ukiendelea kufanyika",amesisitiza CPA Makalla
Amesema kufika eneo hilo ni utekelezaji wa agizo la Rais Dkt.Samia aliyelitoa wakati wa Sherehe za Bulabo zilizofanyika Juni 13,2023 aliyetaka kufanyika kwa mazungumzo ya pande zote ili kufikia mwafaka sahihi.
"Tunakushukuru sana Mhe.Mkuu wetu wa Mkoa kwa hatua hii,nazungumza hapa kwa niaba ya Baba Askofu Renatus Nkwande tulisimama kuja kusali hapa kwa muda wa mwaka mmoja",Padri John Makungu,Paroko wa Parokia ya Kayenze.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.