RC MAKALLA AOMBA JIJI LA MWANZA KUWA NA TIMU YA LIGI KUU
*Asema Mkoa utashughulikia kutafuta timu Daraja la kwanza itakayohamishiwa Jiji*
*Awataka Wadau wa soka kuungana Mwanza upate timu ya Ligi Kuu*
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe.CPA Amos Makalla amewataka Wadau wa soka Mkoani humo kushikamana ili ipatikane timu ya soka ya Ligi Kuu ambayo italeta hadhi ya Jiji hilo na kuinua uchumi kwa ujumla.
Akizungumza leo kwenye kikao cha Baraza la Madiwani wa Jiji la Mwanza, Mkuu huyo wa Mkoa amesema Jiji la Mwanza kwa hadhi yake lina kila sababu ya kuwa na timu ya Ligi Kuu hivyo kawaomba Madiwani kulibeba jambo hilo kwa kushirikiana na Ofisi yake na Wadau kwa ujumla.
"Waheshimiwa Madiwani Mimi ni mpenda soka na nimecheza miaka ya nyuma, hainiingii akilini Jiji hili kukosa timu huku Kigoma na Tabora wakiwa na timu ya Ligi Kuu, iweje Mwanza tukose? Mhe.Meya tafadhali tushikamane katika hili", CPA Makalla
Mkuu huyo wa Mkoa ambaye ni mkereketwa wa mpira wa miguu amebainisha kuwa mchakato wa kupata timu ligi kuu uanzie kufanyika wa kupata timu itakayohamishiwa Mkoani humo kwani Mkoa wa Mwanza una zaidi ya miaka 20 haina timu ya Ligi Kuu.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.