- Adai mamlaka na Wizara kumuongezea muda bila fidia ni kinyume vha utaratibu na sheria
- Serikali mara zote imehaidi kwa wananchi mradi utakamilika Julai 31,2023
- Ataka mkandarasi akatwe fedha za fidia zaidi ya Bilioni 2 ili iwe fundisho.
Mkandarasi anayetekeleza mradi mkubwa wa maji wa Butimba,Kampuni ya Sogea Satom kutoka Ufaransa ametakiwa kulipa adhabu ya kisheria ya malipo ya Shs bilioni 2.5 kutokana na kuzembea kukamilisha mradi huo kwa wakati na badala yake kuongeza muda kinyemela bila uongozi wa Mkoa kujulishwa.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe.CPA Amos Makalla ametoa agizo hilo leo ikiwa ni ahadi yake aliyoitoa wakati wa ziara yake miezi michache iliyopita na kuahidiwa mradi huo kukamilika Julai 31,2023,amesema kitendo cha kuongezewa Mkandarasi miezi mitatu kinyemela ikiwa ni mara ya pili hakikubaliki na ni kwenda kinyume na maagizo ya Rais Samia Suluhu aliyetaka mradi huo kukamilika kwa wakati.
"Hiki kitendo narudia kusema hakikubaliki,ni lazima Mkandarasi huyu akatwe hiyo fidia ili naye fedha hizo zimuume kwani ni dhahiri hatambui wananchi wa Mwanza wanavyotaabika na kukosa huduma hiyo
kwa muda mrefu",amesema CPA Makalla.
Ameiagiza Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jiji Mwanza,MWAUWASA kukaa na Wizara ya maji kuanza kutekeleza mara moja kumkata fedha hizo kwa muda huo wa miezi mitatu ili iwe fundisho kwa Wakandarasi wengine wababaishaji.
"Hili jambo linashangaza sana Mkandarasi amelipwa fedha kwa asilimia 100 mimi nawahaidi wananchi kuanza kupata huduma ya maji ya uhakika kuanzia Julai 31 baada ya kuongezewa muda Februari mwaka huu,huyu Mkandarasi hana sababu yoyote ya kuongezewa muda lakini sasa ni lazima amalizie hiyo miezi 3 pamoja na adhabu hiyo malipo ya fedha kwa kweli sijaridhika kabisa ,"CPA Makalla.
"Mhe.Mkuu wa Mkoa sisi kama MWAUWASA tunakuahidi kuanzia Septemba 15 wananchi wa Mwanza wataanza kupata maji wakati Mkandarasi atakapoanza zoezi la majaribio,hivyo tunaamini changamoto ya ukosefu wa maji kwa wananchi itakwisha,"Mhandisi Robert Lupoja,Kaimu Mkurugenzi MWAUWASA.
Kampuni ya Sogea Satom imeanza kutekeleza mradi huo wa maji Butimba wenye gharama ya Shs bilioni 70 kuanzia mwaka 2021 huku uzalishaji wa maji kwa Mkoa wa Mwanza ukiwa ni lita milioni 90 kwa siku na mahitaji halisi ni lita milioni 160 kwa siku na kukiwa na upungufu wa zaidi ya lita milioni 60.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.