RC MAKALLA ASEMA UJENZI WA JENGO LA ABIRIA UWANJA WA NDEGE UMEKABIDHIWA MAMLAKA YA VIWANJA VYA NDEGE
*Asema ujenzi uliofanyika umekuwa na kasoro nyingi na kutokukidhi viwango vya kimataifa*
*Kukamilika kwa jengo la abiria kutasaidia Mwanza kuwa na Uwanja wa kimataifa*
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. CPA. Amos Makalla amesema mchakato wa ujenzi wa Jengo la Abiria la uwanja wa ndege tayari umekabidhiwa kwa Mamlaka ya viwanja vya ndege (TAA) ili ukamilishwe kitaalmu zaidi na wahusika.
Mhe. CPA. Makalla amesema hayo wakati wa Mkutano wa Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza kujadili hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) leo Juni 26, 2023 katika ukumbi wa Halmashauri hiyo.
"Ni dhahiri uwanja huo ulikosewa sana katika ujenzi wa awali hivyo Ofisi yangu kwa kushirikiana na kamati ya ulinzi na Usalama tumewakabidhi TAA",amesisitiza Mkuu huyo wa Mkoa.
"Tujitahidi sana kutoa ushirikiano wakati wa ufunguzi wa ukaguzi na namna ya kuzipunguza hoja ni nyinyi wenyewe na madiwani wamsikilize mkaguzi wa ndani na atakacho kisema mkaguzi wa ndani kifanyiwe kazi," RC Makalla
Aidha, RC Makalla ameisisitiza menejimenti ya Halmashauri ya Jiji la Mwanza kuhakikisha Wafanyabiashara wa eneo la mlango mmoja wanalipa madeni ya kodi wanayodaiwa na wapitie mikataba na nyaraka ziwasilishwe.
Naye, Mkuu wa wilaya ya Nyamagana Mh. Amina Makilagi amesema atahakikisha kwamba hoja ambazo hazijajibiwa zitakuwa ajenda katika vikao vyote vya ulinzi na usalama ili CAG atakaporudi katika vikao vijavyo hoja ziwe zimepungua au zimejiibiwa kabisa.
Vilevile, Kaimu Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Waziri Shabani amesema anatambua ushirikiano alioupata kwa madiwani na wafanyakazi wote wa halamashauri ya jiji la Mwanza ili kuhakikisha hoja za CAG zinakamilishwa kwa mujibu wa sheria.
Hata hivyo, Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza Mhe. Sima Constantine amesema tunatumaini kadri siku zinavyozidi kwenda Halamashauri yetu hii ipo siku itasimama pasipokuwa na hoja hata moja.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.